KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday, 10 March 2015

DK MTITU ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

DK MTITU
VUTANO mkali  ubunge jimbo la Kalenga  baada ya  mpinzani  wa Jackson  Kiswaga   kutoka kata  ya Nzihi Msomi Dr Evaristo Mtitu   kutangaza  nia ya  kugombea  ubunge katika   jimbo la Kalenga  linaloongozwa na Godfrey Mgimwa (CCM).
 
 
Akizungumza na mtandao wa www.matukiodaima.co.tz Dr. Evaristo Andreas Mtitu alisema  kuwa amelazimika  kujitokeza  kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka huu kupitia  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (Chadema)Dr  Mtitu alisema  kuwa  yeye ni   mzaliwa Kidamali kata ya  Nzihi katika  halmashauri ya  wilaya ya  Iringa alizaliwa  mwaka  (1974)  na  kusoma  Shule ya msingi Nyamihuu  Olevel Ulayasi Secondary 1995. 

 Alevel Mzumbe High School Morogoro 1998,
Pia  baada ya  hapo alijiunga na   Stashahada ya ualimu  Chuo cha ualimu Morogoro 2001. Shahada  ya kwanza ya Elimu,  Chuo kikuu DSM,  2006.  Shahada ya uzamili katika elimu,  Chuo Kikuu cha Charles Darwin,  Australia,  2009.  
 
Dr Mtitu pia  alisema amehitimu Shahada ya uzamivu (Doctor of Philosophy) katika elimu Chuo Kikuu cha VICTORIA cha Wellington,  New Zealand,   2014.
 
Akielezea  kazi ambazo amepata  kufanya  katika  nchi  kuwa ni pamoja na ualimu Shule za sekondari , mkufunzi vyuo vya ualimu Tandala na Klerruu huku kwa  sasa  ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania aliyebobeakatika taaluma ya mitaala ya elimu na ufundishaji,
 
Katika  Nyanja  ya   utandawazi alisema  yeye ni mtafiti, elimu ya Geography,  sera mipango na uongozi katika elimu na nadharia ya upembuzi.
 
Hivyo  alisema  kuwa  lengo  lake la  kutaka   ubunge  jimbo la  kalenga ni  kushirikiana na  wana Kalenga  katika  kuleta maendeleo .
 
Kipaumbele  chake ni  kuboresha   elimu na  huduma  za  afya ,miundo mbinu  huku akimpongeza  mbunge  wa  sasa  Bw Mgimwa  kuwa amejitahidi  kufanya  kazi  kulingana na  uwezo  wake  kwa  muda  mfupi ila bado  kuna  haja  ya  kumuunga  mkono kwa  kumsaidia  zaidi kwa  kuliunganisha  jimbo   hilo na  wahisani  wa  ndani na  nje.
 
Kujitokeza  kwa Dr  Mtitu  katika  kata  hiyo ya  Nzihi  kutafanya kata  moja   hiyo kuwa na wagombea   watatu  hadi  sasa  wanaotaka  ubunge  kutoka kata  hiyo .

No comments:

Post a Comment