WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesitisha
uingizaji wa mabewa 124 yaliyobaki kutoka nchini India hadi atakapopata ripoti
ya uchunguzi wa mabewa ya mizigo 150 yaliyochini utakapokamilika.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Sitta, alisema kama kuna watendaji wamefikia hatua ya kuingiza
mabehewa yaliyochini ya kiwango basi hiyo ni sawa na hujuma.
Alisema kuwa uchunguzi wa mabehewa hayo 150 ulikuwa
ukifanywa na Kamati Uchunguzi iliyoundwa na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Dk.
Harrison Mwakyembe, unatarajiwa kukamilika siku ya Ijumaa Machi 13 mwaka huu.
“Waziri aliyenitangulia aliteua kamati kupitia
Bodi nisema kuwa uwamuzi huu ni sahii na mimi na unga mkono kwani uamuzi huu unatokana na ukweli kwamba mabehewa haya kuwa
makuu hali inayosabisha mabehewa hayo kuwanguka kwa wastani wa Desemba mwaka
jana yalikuwa yakianguka kila siku yawapo njiani hali inayosababisha hasara kwa
nchi.
“Nimemuagiza Mwenyekiti wa Bodi Bodi ya TRL
kukutana na Kamati ya uchunguzi siku ya Ijumaa ili kupitia taarifa hiyo na
watakapomaliza wahakikishe kuwa hadi
Ijuma 16 iwe imenifikia ofisini kwangu ili kupata taarifa kamili kuhusu
mabewa haya,”alisema Sitta.
Sitta alisema endapo taarifa ya uchunguzi huo
itabainisha kuwa kulikuwa na ubabaishaji katika manunuzi ya mabehewa hayo 150,
Serikali haita sita kuvunja mkataba huo
kwa kutumia sheria ya manunuzi.
Aliema licha ya kuvunja mkataba huo pia
kunauwezekano mkubwa kumshitaki mhusika, kuaangalia kuwa ni nani mwingine
amehusika kwenda kuangalia mabehewa hayo na kufikia hatua ya kupewa mabehewa
hayo mabovu.
Alisema ikishindikana kuvunja mkataba huo basi
itabidi wahusika walazimishwe kusimamia gharama za matengenezo ya mabehewa hayo
ambayo tayari yamekwisha ingizwa nchi.
Sitta, alisema pia Serikali itaangalia ni nani
alihusika kwenda kukagua kasha akakubali nchi ipate kitu kibovu, akibainika
kutokana, uzembe huo na kuliletea hasara taifabasi ili aweze kuchukuliwa hatua
za kisheri.
Aidha, alisema kuwa hali ya Shirika hili
inazidi kuwa bora siku hadi siku hususani katika upande wa mapato.
Sitta, alisema katika kipindi cha Desemba mwaka
jana, Shirika limeweza kuzalisha kiwango cha dola za kimarekani 140
ukilinganisha na kiwango cha dola 30 Junuari huo huo, ambacho hicho ndio cha
chini kabisa.
“Pia tumepata taarifa kuwa hali ya usafiri wa
abiria unazidi kuimarika kwani hivi sasa kuna vichwa 60 ambapo mahitaji ni
vichwa 107 lakini kwa kuwa na hivi hali si mbaya,”alisema Sitta.
Akizungumzia kuhusu watumishi, Sitta, alisema
watumishi wanapaswa kulipwa kama mikataba yao inavyoonesha katika makubaliano
yao.
No comments:
Post a Comment