![]() |
| Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Natty |
BAADHI
ya Wananchi wa Mtaa wa Madale Kata ya Wazo wilayani Kinondoni mkoani Dar
es Salaam wametaka uchunguzi ufanyike haraka na kuwafikisha mahakamani watu wote waliohujumu mradi wa maji wa Madale.
Pia
wametaka mradi huo ulirudishwe katika Kampuni ya Majisafi na Majitaka (Dawasco).
Wakizungumza
katika mkutano wa hadhara Dar es Salaam jana, wananchi hao walisema
inasikitisha kuona kuwa Dawasco inawauzia uniti moja ya maji kwa
sh.1200 lakini wao wanauza uniti moja ya maji kwa sh.5000
Walisema maji yaho yamekuwa yakiwanufaisha
wachache huku mamilioni ya shilingi yakiliwa na watu wachache ambapo
Kamati ya awali iliyokuwa ikisimamia maji imefanya ubadhirifu mkubwa huku.
Walisema
licha ya kamati hiyo kufanya ubadhirifu bado wapo baadhi ya Viongozi ambao
wamekuwa wakiwakingia vifua awali, lakini sasa wamechoka na wameamua
kuteua Kamati mpya.
Wananchi
hao walisema wakati mradi huo unaanzishwa katika eneo hilo, walishiriki
kuchimba msingi na hadi ukamilike ulihitaji sh. milioni 500 lakini Mwenyekiti
wao kwa kushirikiana na viongozi wengine waliendesha harambee na
kufanikiwa kupata fedha kwa asilimia 95.
Walisema ni lazima ukaguzi ufanyike juu ya
Kamati iliyopewa jukumu la kusimia mradi huo na kisha wakabidhi
nyaraka zote na wakibainika kuhusika na hujuma dhidi ya mradi huo basi ni lazima wafikishwe
mahakaman
Walisema licha ya kujitahidi na kufanikisha
suala hilo lakini bado wanapata maji mara moja kwa wiki au mbili wakati wenzao wengine wanapata maji kila
siku hivyo kuanzia siku hiyo hawaitaki tena Kamati hiyo na sasa wanakamati mpya inayoongozwa na
Amina Kawawa.
"Cha
kushangaza zaidi wanaonufaika na maji ni wageni ambao hata shilingi
hawajachangia lakini waliochimba mitaro hawana hata tone la maji na kwa
haya maji yapo kilomita 50 tu kutoka yalipo lakini bomba hilo hilo
linapeleka maji.
Kigamboni
na wao wananunua kwa bei rahisi kabisa iweje sisi hapa"alisema
Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina Rashid Mkali.
Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina
moja la Mlay alisema yeye alitoa zaidi ya sh. 400,000 kwa Kamati ya Maji
ya Madale lakini tangu amelipia hajawahi kupata maji hayo hadi leo hiizaidi
ya kutoka mara mbili jambo ambalo linamshangaza.
"Hawana hata huruma wamekuja nimewapa zaidi
ya sh.400000 ili waniunganishie maji lakini cha ajabu maji hayatoki
na kila mwisho wa mwezi wanakuja kusoma bili yao sasa nawauliza tangu mnifungie
bomba hapa zaidi ya miezi mitano iliyopita sijapata maji leo mnakuja
kusoma nini hapa"alisema Mlay.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo
Grasian Mbelwa alisema wao walifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Waziri
Mkuu Mstaafu Rashid Kawawa kuhakikisha kuwa watu wa Madale wanapata
maji lakini mradi huo umehujumiwa kwa kiasi kikubwa.
"CCM haiwapendi watu wanouumiza wananchi
bali inataka watu wanaoleta maendeleo katika jamii hivyo basi kwa
kuwa wananchi wenyewe ndio mmewapendekeza watu wanaounda Kamati Mpya ya
Maji basi mimi kama Serikali ya Mtaa nitatoa ushirikiano wa kutosha
kuhakikisha kuwa Kamati hii inafanya kazi yake alisema Mbelwa.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi mbambali wa Vyama
vya Siasa kikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama
cha Wananchi (CUF) huku wananchi hao wakimpongeza Mwenyekiti huyo kwa
kuitisha mikutano ya hadhara na wananchi kupata fusra ya kuzungumzia fursa
za maendeleo katika mtaa wao.

No comments:
Post a Comment