HOSPITALI ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa magodoro 50 yenye thamani ya sh. milioni 5 kutoka kwa Citizen Foundation.
Akikabidhi msaada huo mwishini mwa wiki kwa Mganga Mfawidhi, Dk. Amani Malima, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Citizen Foundation, Lilian Wassira, alisema ameamua kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada wa magodoro kwa ajili ya mama wajawazito.
Alisema hakuona haja ya kukodi kumbi za starehe na kufanya starehe ilhali wajawazito wakitaabika hospitalini kwa kulala chini kutokana na uhaba wa magodoro na vitanda.
Lilian, lisema wameandaa harambee ya maalum ya kitaifa kwa wabunge wote watakaopanda jukwaani kuomba kura ambapo watawapelekea barua za kuchangia huduma za afya.
"Atakayechangia kwenye harambee hiyo tutamtangaza kwa umma ili wajue yuko karibu na jamii huku wale wasiochangia nao watatangazwa ili wanyimwe kura," alisema.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk.Amani Malima, alisema hospitali hiyo inahitaji vifaa mbalimbali hivyo ni vyema kila Mtanzania mzalendo akajitolea kuisaidia.
Kwa siku tunalaza wagonjwa 370 hadi 400, vitanda vilivyopo ni 340, tunahitaji vitanda 250 kwa sababu kwa siku tunapokea idadi kubwa ya wagonjwa, pamoja na uhitaji huo bado tuna changamoto ya eneo ni dogo,îalisema Malima.
No comments:
Post a Comment