KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 9 March 2015

VODA YAZINDUA HUDUMA NPYA YA KUTUMA FEDHA KENYA


KAMPUNI ya simu za mikononi Vodacom imezindua huduma ya kimataifa ya kutuma  pesa nchini Kenya (IMT), ambayo itawawezesha wateja wake wa Kenya 300,000 wanaoishi nchini kutuma pesa kupitia mtandao wa Safaricom.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza alisema zaidi ya wateja milioni saba wa hapa nyumbani wataweza kukamilisha miamala yao kwenda nchini Kenya.

Alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo kumetokana na utafiti walioufanya na kubaini kuwa wengi wamekuwa wakipata shida katika utumaji wa fedha hali inayowafanya wengine watumie njia za kienyeji ambazo si salama.

Naye Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu, Bernad Dad alisema mfumo huo utawasaidia Watanzania kupokea na kutuma fedha kwenda nchini Kenya kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii na biashara.

Kuhusu viwango vya kutuma, alisema vitakuwa sawa kama vile unavyotuma kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hapa nyumbani na kutoa angalizo kuwa biashara hiyo ni lazima iendane na sheria ya nchi husika.


No comments:

Post a Comment