MWENYEKITI wa Chama cha Mabadiliko
na Uwazi (ACT-Tanzania), Kadawi Limbu, amemtaka mwanachama mpya wa chama hicho Zitto
Kabwe, kuachana na mawazo ya kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu hadi atakapotimiza miezi sita ya
uwanachama wake.
Limbu ambaye anapinga
kuondolewa kwenye nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho alitoa kauli hiyo wakati
alipozungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Mimi bado ndio mwanyekiti wa
ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwa kuniondoa katika nafasi ya uenyekiti haikuwa
halali na ili nifanya kupeleka suala hilo mahakamani kwa ajili ya kupata
muongozo,”alisema Limbu.
Limbu, alisema hivyo kwa vile
katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka
kugombea nafasi yoyote ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi
ya miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.
“Mkiangalia mtaona Zitto
ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata, katiba
haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu ni muombe kwamba andelee
kuwa mwanachama wakawaida tu,”alisema Limbu.
Hata hivyo, mwenyekiti huyo,
alimtaka Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha
wanachama kuhusu uchaguzi huo kwani uchaguzi
huo siyo halali kutokana na mwenyekiti huyo kwena mahakamai kupinga kuondolewa
katika nafasi hiyo.
Akizungumzia chanzo cha mgogoro
huo, Limbu alisema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, kutokana naofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa taarifa zinazochanganya
katika vyama.
Aliwataka wanachama wa chama
hicho kutambua kuwa msajili huyo siyo anayepanga uongozi ndani ya vyama vya
siasa.
Limbu alidai kuwa ameamua
kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasi ya Kuuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia kuwa
mwenyekiti wa chama hicho.
Limbu alitoa angalizo kwamba
atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama kubwa
kukiona kikiangukia mikononi mwa mafisadi.
Alisema kuna watu wanajiita
wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya
kunyang’anya haki za haki za watu, watu hao ni sawa na majambazi.
Msemaji wa ACT-Tanzania,
Abdallah Khamis, alisema katiba ya chama hicho, iliyoko kwa Msajili wa Vyama
vya Siasa, inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yeyote ya
uongozi endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.
Pia alisema kuwa uchaguzi huo
utafanyika kama ulivyopangwa kwa vile chama hicho hakina mgogoro wa kiuongozi
mahakamani bali wanachojua shauri lililoko mahakamani ni la mtu binafsi.
“Huyu sio mwenyekiti tena wa
chama chetu naomba muelewe hivyo amejiita mwenyekiti atakuwa amefanya makosa na
kuna hatari ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kuweni makini naye,”alisema
Khamis.
Khamis, alimuonya aliyekuwa
mwenyekiti wa muda wa chama hicho kuacha kupitapita mitaani na kuwapotosha
wanachama badala yake kama anataka kuwa kiongozi ajipange kugombea na yeyote
katika uchaguzi huo Mach 28 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment