KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 15 March 2015

MCHUNGAJI MABILE APORA ARDHI NA KUIUZA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MWENYEKITI wa Kijiji cha Nyakasangwe Kata ya Wazo wilayani Kinondoni, Peter Mibilale anadaiwa kupora ardhi ya mkazi wa kijiji hicho, Claud Chikonyi, kuingia katika makubaliano ya kuiuza kwa mtu ambaye hakujua kama alikuwa akimchunguza.
 Mgogoro huo ulianza Feburuari 21 mwaka huu baada ya Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste, kudai kuwa eneo analomiliki Chikonyi, lilitengwa maalumu kwa ajili ya huduma za kijamii.
 Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Chikonyi, alisema eneo aliloporwa na mwenyekiti huyo, analimiliki tangu mwaka 2001, hata kabla mwenyekiti huyo hajahamia kijijini hapo.
Alisema, baada yakuporwa eneo lake aliwatafuta waandishi wa habari, ambao walifanya uchunguzi kwa mmoja wao kujigeuza mteja anayetafuta eneo la kununua katika kijiji hicho ndipo mwenyekiti huyo alipojitokeza na kuingia makubaliano ya kuuza kipande hicho cha ardhi, alichodaiwa kukipora kwa Chikonyi.

 “Baada ya kuaniandikia barua ya kunitaka niache mara moja kufanya shughuli zamaendeleoo katika eneo langu kabla hata hajakutana na mimi ndio akaamua kuliuza kwa kwa gharama ya sh milioni 4 cha kushangaza alitoa Namba Akaunti ya ndugu yake,”alisema Chikonyi.Chikonyi, alisema vielelezo vyote vya makubaliano ya kuuzwa eneo hilo vipo ikiwemo wajumbe ambao walishuhudia zoezi hilo wapo.
“Nasikitika kama kiongozi aliyechaguliwa kwa nia ya kusaidia kutatua matatizo yanayojitokeza katika jamii leo yeye ndiyoanakuwa wakwanza kuwavuruga wananchi, sasa wananchi watakimbilia wapi watakakopata haki zao,”alisema Chikonyi.
Ofisa Ardhi wa Manispaa hiyo, Jermia Masinga alisema hakuna sheria inayomruhusu Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kugawa ardhi, hata kama serikali ikiamua kuchukua eneo la mwananchi lazima afidiwe.
Alisema wanaohusika kugawa ardhi ni Kamati ya Wilaya ambayo Mwenyekiti wake ni Mkurugenzi huku Meya akiwa Katibu.
Masinga, alisema kama kweli mtu huyo amefikia hatua hiyo basi achukuliwe kuwa ni mhalifu, anayedai kuporwa eneo lake achukue hatua za kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kama wahalifu wengine.
Hata hivyo, Mchungaji huyo alipogiwa simu na waandishi hao na kuelezwa madai hayo alikata simu hata alipopigiwa tena simu iliita kwa muda mrefu hadi kukatika yenyewe.


No comments:

Post a Comment