![]() |
| Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo |
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema mfumuko wa bei wa Taifa umeongezeka
kutoka asilimia 4.0 katika kipindi cha Januari hadi asilimia 4.2, Februari
mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo, alisema Fahiri za bei
zimeongezeka kutoka 148.62 Februari, 2014 hadi 154.83 kwa Februari mwaka huu.
Alisema hali hiyo imetokana na kasi ya upandaji wa bei za
bidhaa na huduma kwa mwaka uliyoishia Februari mwaka huu, imeongezeka
ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka uliyoishia Januari mwaka huu.
Kwesigabo, alitaja baadhi ya bidhaa za vyakula
zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi, zikiwa na asilimia yake ndani ya mabano
kuwa ni pamoja ni mchele (5.0), samaki (3.0), matunda aina ya machungwa (7.7),
ndizi za kupika (2.6) na mbogamboga (5.3).
Nyingine ni baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula ambapo
zilichangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mkaa (11.5), vyombo vya jikoni
vya aina ya kioo (2.5) na vyakula vya migahawani (1.5).
Kuhusu thamani ya
shilingi ya Tanzania
Kwesigambo, alisema thamani ya shilingi inatafriwa kuwa
ni badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma
zilezile za mlaji ambazo shilingi hiyo ingeweza kununua katika vipindi tofauti
“Ikiwa wastani wa fahirisi za bei za taifa unaongezeka,
uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua,”alisema
Kwesigabo.
Aidha, alisema uwezo wa sh. 100 ya Tanzania katika kununua
bidhaa na huduma umeshuka hadi sh. 64.59 mwezi Februari mwaka huu kutoka
Septemba mwaka 2010.

No comments:
Post a Comment