NA MWANDISHI WETU
MRADI wa
mawasiliano kwa wakulima nchini unaojulikana kwa jina la Mkulima Mbunifu,
unatarajia kutoa mafunzo ya Kilimo Hai, ya siku mbili kuanzia Machi 30 hadi 31
mwaka huu mkoani Arusha.
Kwa
mujibu Msimamizi wa Mradi huo Tanzania, Ayubu Nnko, mradi huo unasimamiwa na Biovision
Africa Trust, kwa ufadhili wa Shirika la Biovisior Foundation for Ecological
Development, Switzerland.
Alisema
mafunzo hayo ya siku mbili yatajumuisha wandishi wa habari za kilimo na
mazingira pamoja na wadau wengine wa kilimo na ufugaji.
“Hawa ni
wadau ambao kwa namna moja au nyingine wanashiriki katika kueneza na kutoa
elimu ya kilimo endelevu nchini,”alisema Nnko.
Nnko, alisema
katika kufikisha elimu kwa walengwa mradi huo unachapisha na kusambaza jarida
la lijilikanalo kwa jina la Mkulima Mbunifu, pamoja na machapisho mengine kwa
vikundi vya wakulima hapa nchini na baadhi ya maeneo ya nchi jirani
zinazopakana na Tanzania.
Pia
wanatayarisha vipindi mbalimbali vya redio vinavyorushwa kupitia Shirika la
Utangazaji nchini TBC Taifa na Sauti ya Injili Moshi.
“Huduma
hii hutolewa bure kwa vikundi vya wakulima na taasisi zinazojishughulisha na
kilimo endelevu,”alisema Nnko.

No comments:
Post a Comment