BAADHI ya madereva na abiria wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kutotuama maji eneo la Kituo cha daladala Akiba pindi mvua zinaponyesha.
Wadau hao wa usafiri walisema hivyo baada ya mvua iliyonyesha kuanzia jana na leo Alfajiri, kusababisha eneo hilo kujaa maji hadi madereva kushindwa kushusha abiria katika kituo hicho.
Walisema kama hakutapatikana ufumbuzi wa kudumu ambao utasidia kudhibiti maji katika eneo hilo, basi watafute utaratibu utakaowafanya wasimamishe magari yao nyuma kidogo ya kituo hicho.
Wadau hao walisema hivyo ili kuepuka kukamatwa na polisi pindi wanaposima mbali na kituo hicho wakati kinapojaa maji hususan nyakati kama hizi.
Eneo hilo limekuwa korofi kwa kujaa maji kwa pindi kirefu huku wahandisi wakishindwa kubuni njia ambazo zingesaidia kuzuia maji yasituame katika kituo kile.
Kujaa maji katika eneo hilo, kunasababisha kero kubwa kwa watu wengi wenye vyombo vya moto pia watembea kwa miguu,.
Walisema kuna kipindi watembea kwa miguu wanshindwa kutembea kwa uhuru huku wakati mwingine kufikia hatu baadhi ya watembea kwa miguu huvushwa katika eneo hilo kwa kubebwa na vijana kisha hulipa kiasi chochote.

No comments:
Post a Comment