KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 18 March 2015

MWALIMU WA KINYESI HAJAONEKANA

MMLIKI wa nyumba aliyokuwa akiishi Mwalimu wa shule ya Sekondari Kibasila Gaudensia Albert aliyekutwa na mrundikano wa kinyesi chumbani kwake, Reuben Shayo, amesema hajamuona mwalimu huyo tangu kutokea tukio hilo mwezi mmoja uliyopita.

Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Kisiwani Kata ya Sandari wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini leo, Shayo alisema kutoonekana kwa mwalimu huyo hakumtii wa wasiwasi kwani hadi sasa vyombo vyake viko katika hali ya usalama pia hana deni analomdai.
Alisema, hivyo kwa vile haoni haja ya kumtafuta mwalimu huyo kwani hana deni analodai ambapo hadi sasa mwalimu huyo anamkataba wakuishi katika chumba hicho hadi Juni mwaka huu.

Alisema, baada ya kumalizika mkataba wake kama hataonekana basi atatumia njia alizotumia awali za kuwatafuta viongozi wa serikali ya mtaa na polisi ili kutoa vyombo vyake.

“Unajua hata tulipokiteketeza ule mrundikano wa kinyesi kilichochanganyika na matapishi na mikojo ilibidi tuvunje mlango kwa kutumia nguvu ya dola kwa ajili ya usalama wa vyombo vyake na tulipomaliza kuvunja lilinunuliwa kufuli jipya ambalo ndio limebana mlango wa chumba hicho cha mwalimu na funguo ziko kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Yahya Bwanga,”alisema Shayo.

Mkuu wa Shule Msaidi, Frida Kyando, alipoulizwa kama mwalimu huyo anaonekana shuleni hapo, alisema tangu zilipozagaa taarifa hizo alipatwa na mshtuko ambao umemfanya aplekwe hospitali ya Temeke baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Kwani mkataba wake wa kupanga hicho chumba umeisha basi kama bado hakuna tatizo,:alisema Frida.

Frida, alisema hivi sasa mwalimu Gaudensi bado amelazwa katika Hospitali hiyo, akidai kuwa yuko katika hali mbaya.

Mwezi mmoja uliyopita katika chumba anachoishi mwalimu huyo kuligundulika mlundikano wa kinyesi kilichokuwa kimehifadhiwa katika ndoo za plastiki, mabeseni, chupa za chain a soda, na vyombo vingine vyote vikiwa vimejaa kinyesi hicho kilichohifadhiwa kwa muda wa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment