KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday, 17 March 2015

UWWADA WATAKIWA KUJIUNGA NSSF

UMOJA wa Wafanyabiashara Walemavu Dar es Salaam (UWAWADA), umemshutumu  mmoja wa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja huo, David Nyendo, kujipatia mkopo wa sh milioni 500 kwa kutumia Saccos ya walemavu.

Wakati Nyendo akishutumiwa, naye amefunguka akisema wanaodai hivyo hawajui chochote kuhusu kunachoendelea katika upatikanaji wa mikopo hiyo.
Nyendo, aliondolewa madarakani miaka mitatu iliyopita baada ya kutokea vurugu kubwa za kupinga uongozi wake, hata hivyo,  inadaiwa wakati anaondoka, aliondoka na baadhi ya nyaraka za Saccos hiyo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini leo, Mwenyekiti wa Umoja huo Mohamed Kidumke, alisema kitendo alichofanya Nyendo ni cha kikatili kwani anajua changamoto zinazo wakabili walemavu wenzake.

“Hii Saccos ilifungwa baada ya Saccos hiyo kuyumba hadi kushindwa kuwaapatia mikopo wanachama wake pia pango la ofisi na kuzuiliwa vyombo vyake na mmiliki wa nyumba,”alisema.
Alisema, mwaka jana Nyendo alitumia fojali kwa kuomba mkopowa sh. 200 kwa kutumia nyaraka za umoja huo kwa maslahi yake binafsi pamoja na rafiki yake.

Kidumke, alisema mkopo huo aliutumia kwa kunulia Bajaji na gari ambazo hakuzitaja idai yake, alizozitumia kufanya biashara ya kusafirisha abiria (Daladala).

Alisema kutoka na biashara zake hizo alifanikiwa kurejesha mkopo huo kwa wakati, ambapo alichukuwa mwingine wa milioni 307.
Kwa upande wake Nyendo, alisema hao wamekosea, kwanza wanaotoa madai hayao ni watu wachache ambao hawajui kinachoendelea.

Alisema mkopo unaotolewa na NSSF hautolewi kwa Saccos Walemavu kama wanavyo dhani ni kwa ni wanachama wa sakosi hiyo ambao wamechangia michango yao katika mfuko huo wa NSSF kwa zaidi ya miezi sita.

“Ili mwanachama atambulike ni lazima awe anachangia michango yake kila mwezi na katika kupatiwa mkopo ni lazima iangaliwe kiasi alichochangia pia mkopo huo utaenda na dhamana.

“Sijatumia fojali kama walivyosema, unajua baada ya Saccos ile kuyumba mwaka 2012 ilibidi iundwe nyingine mwaka 2013 sasa cha msingi wanachotakiwa ni kujiunga na sakosi hiyo na kuanza kuchangia NSS  kupitia Saccos yetu,”alisema Nyendo.

Nyendo alisema katika mkutano kati ya Uwawada, Katibu tawala wa Mkoa na Maofisa Ushirika wa Ilala na Temeke, walikubaliana kuwa wanachama wa Uwawada kuanzia sasa waanze  kujiunga na Saccos hiyo kisha walipe michango yao, baada ya kutimiza miezi sita wataangaliwa na wataalamu wa NSSF kama wametiza vigezo.

No comments:

Post a Comment