KITENGO cha Vijana wa Chama cha NCCR Mageuzi, kimempendekeza
Dk. George Kahangwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Uwamuzi wa Kitengo hicho haumzui mwanachama mwingine wa
chama hicho kujitokeza na kuomba kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo kwa niaba ya
vijana wenzake, Mwenyekiti wa kitengo hicho, Deo Meck amesema wamefikia umauzi
huo baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu ndani ya chama kuhusu mgombea
anayefaha.
Amesema, kutokana na mazoea kwamba wagombea wa nafasi
mbalimbali hujitokeza wao wenyewe, lakini kitengo hicho kimekuwa tofauti baada
ya kushiriki kumtafuta mgombea urais atakaye peperusha bendera ya chama na
kuliletea taifa mabadiliko chanaya.
“Tuliona tutafute mtu anayekidhi vigezo vya kutosha vya
kikatiba, mwenye sifa zinazotajwa na chama ambazo ni uwezo, ucha mungu, kuchukia
ufisadi na awe mzalendo asiyetiliwa shaka,”alisema.
Amesema kwamba mbali ya kumuomba agombee, pia wanamtaka akubaliane
na pendekezo lao la kumchukulia fomu ya chama na kumlipia ada inayotakiwa pindi
wakati utakapowadaia.
Halladhalika wameshindwa kupendekeza jina la Mwenyekiti wa
chama hicho James Mbatia, kwa vile tayari amekwisha tangaza nia ya kugombea
ubunge katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
“Tutafanya jitihada na kuhakikisha jina lake linafika
katika kikao cha Halmashauri ya chama, ili lipewe baraka za mkutano mkuu wa
chama, hatimaye kushindanishwa na wagombea wengine watakaosimamishwa na vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuwa mgombea wa ngazi ya
urais,”alisema.
Akitaja wasifu wa Dk.Kahangwa amesema ni Mhadhiri wa
Chuo Kikuu
Dar es Salaam kampasi ya Mlimani, ambaye anafanya tafiti kufundisha na kutoa
huduma kwa jamii katika masuala ya uongozi, sera na mipango hususan ya elimu.
“Alipata shahada yake ya kwanza chuoni hapo mwaka 2004,
ambapo alipata ufaulu wa juu na kuibuka mwanafunzi bora wa kitivo, pia
alihitimu mafunzo ya uongozi katika taasisi ya Kijerumani iitwayo Fredrich
Ebert Stiftung (FES),”.
Mbali na hayo ni mhitimu wa shahada ya uzamivu (udakltari
falsafa), katika Chuo cha Briston Uingereza, pamoja na kusomea masuala ya
kimataifa katika chuo cha Oulu nchini Finland.
Kuhusu uzoefu wa kisiasa, Dk.Kahangwa aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkuu wa Idara ya
Itikadi, Sera na Mafunzo pamoja na kuwa Makamu Mkuu wa chuo cha chama.
Alitaja sifa zilizochangia kumpendekeza Dk.Kahangwa, amesema wamezingatia umri, elimu, uzalendo na
kashfa za kisiasa ndio maana wamempendekeza.
“Hakuwahi kuwa na kashfa yoyote ya kisiasa ni msafi hana
hata doa, pia kiwango chake cha elimu kipo juu, hata hivyo ana uzalendo na
uwezo wa kuliongoza taifa licha ya kuwa hana umaarufu wa kutisha,”amesema.
Hata hivyo, amesema kwamba hawamnyimi nafasi mwanachama
yoyote anayetaka kuwania nafasi hiyo, kwani uamuzi walioufanya wao ni
kupendekeza mgombea wakiwa kama vijana waliokuwa ndani ya chama.
No comments:
Post a Comment