WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara
nchini (Tanroads), Injinia Peter Mfugale, kuzikabidhi barabara zilizokamilika
za mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) ili ziweze kufunguliwa na kutumika.
Dk.
Magufuli alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kuweka
jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Uhuru pamoja na kufanya
ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi hayo katika barabara ya Morocco –
Magomeni - Fire hadi Kariakoo.
Dk.
Magufuli alisema wakazi wa jiji hilo wana hamu ya kuona barabara hizo
zilizokamilika zinafunguliwa na kutumika ili kupunguza msongamano wa magari
yaliyomo katika jiji hilo.
“Sisi
kazi yetu ni kujenga lakini wenye majukumu ya kuzifungua ni Wizara ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), sasa namuagiza mtendaji mkuu wa Tanroads
kukabidhi barabara zote zilizokamilika ili waweze kuzifungua kwa kuzingatia
masharti yake ya kuingiza mabasi makubwa,” alisema.
Dk.
Magufuli aliitaka Kampuni ya ujenzi wa mradi huo (Strabag), kuanzia sasa ifanye
kazi usiku na mchana ili kukamilisha sehemu ya ujenzi huo kwa ajili ya barabara
hiyo kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kabla hajamaliza muda wake mwishoni mwa
mwaka huu.
Alisema
kwa kuwa Rais Kikwete aliahidi kuwaachia mradi huo ukiwa umekamilika hivyo
halitakuwa jambo jema kama ataondoka kabla haujakamilika.
Akizungumzia
upanuzi wa Barabara ya Uhuru hadi Buguruni Malapa, Dk. Magufuli alisema
barabara hiyo ina urefu wa kilomita tatu ambapo itakuwa ya njia nne.
“Hii ni
barabara yenye historia ndefu na ambayo imekuwa na matumizi makubwa ikiwemo
kutumiwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje wanapofanya ziara nchini,”
alisema.
Alisema
ujenzi wa barabara hiyo kuwa ya njia nne utasaidia kupunguza adha ya foleni
iliyopo sasa.
Mkuu wa
Mkoa, Said Meck Sadik, alikemea vitendo vya uchafu unaofanywa na wakazi wa jiji
hilo, ambapo baadhi yao wamevigeuza vituo vya mabasi vya mradi huo kuwa
‘guest’.
Aliwataka
wananchi kuwa wazalendo kwa kuilinda miundombinu hiyo, kwani ujenzi wake
umetokana na kodi zao.
No comments:
Post a Comment