![]() |
| Mjumbe wa Halmashauri Mkuu CCM Taifa, Mgeja |
MJUMBE wa Halmshauri Kuu ya
CCM Taifa, Khamis Mgeja ameliita kundi la vijana wa zalendo wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kuwa ni genge la vijana linalotumiwa kwa malengo ya mtu
aliyewatuma.
Mgeja alitoa kauli hiyo
baada ya kushtushwa na vijana hao wanaojiita wazalendo wa CCM kutoka Tanzania
Bara na Visiwani, kutoa tamko ambalo linadai kuwa baadhi ya makada wanaotaka
kuwania nafasi ya urais kuonyesha kiburi cha kutofuata sheria na kanuni za
chama licha ya kuonywa mara kwa mara.
Makada
hao, ambao wameonywa na kupewa adhabu ya miezi 12 kwa kuanza kampeni mapema,
Februari 18 mwaka jana ni Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Mahusiano na
Uratibu), Steven Wasira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari
Makamba, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na mawaziri wakuu wastaafu,
Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
“Wao
wanapodai kuna makundi ndani ya chama kwa kauli hiyo basi nao wajue tayari
wamekwishaanzisha ubaguzi, ila wajue makundi wakati wa uchaguzi ni jambo kawaida
ili mradi hayahasimiani, pindi uchaguzi unapokwisha nayo hutoweka,”alisema
Mgeja.
Megeja,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, alisema hivyo kwa vile genge
hilo ndani ya
chama haliko kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
“Genge
hilo ni la watu, unaona bwana, hawa ni vijana
ambao wamekuswanywa wakitumiwa kwa malengo ya mtu yaliyewatuma, tunajuana hawa
wanatumika kinyume na maelezo yao,”alisema
Mgeja
Alisema
chama ni vikao kama wao wanaagenda yao
nzuri waiwasilishe kwenye vikao halali vya chama lakini cham hakiwezi kujengwa
na agenda za watu ambao hawajulikani.
“Kitendo
wanachotumia ni sawa na kumtishia mtu mzima nyau hao waache kuwatishiwa watu
wazima nyau, wao kama wana ubavu na hoja waseme
lakini wajue chama kuanzia ngazi chini hakina mgongano, wasiwape hofu wanachama
nchini,”alisema Mgeja.
Alisema
kama kweli wao ni wazalendo basi watumie nguvu zao kueneza mazuri yaliyofanywa
na chama chao chini ya Rais Jakaya Kikwete, lakini siyo vyema wakadandia treni
wasilolijua.
Mgeja,
aliwataka vijana kutambua kuwa chama hakiwezi kujengwa nje ya chama hivyo ni
vema vijana hao wakajenga hoja zao kisha waziwasilishe katika vikao halali,
akiamini kuwa watasikilizwa.
Alisema
ni jambo la hatari kwa baadhi ya wanachama kuanzisha makundi kama hilo la wazalendo ndani
ya chama kitendo hicho kinaweza kuleta mpasuko wa chama jambo ambalo haliombei.
“Kwa
kuwa na kundi la wazalendo na kundi ambalo sio wazelendo hili ni pepo baya kwa
mustakabali wa chama, linafaa likemewe,”alisema Mgeja.
Hivi
karibuni Mwenyekiti wa vijana wa zalendo wa CCM, Hassan Marijan, alikaririwa na
vyombo akisema kuwa wameshuhudia kundi fulani la makada ambao wanatumia mwanya
wa kuwashawishiwa kugombea Urais.
Alisema
makada hao wamekuwa wakiandaa makundi mbalimbali ya kijamii kwa mkono wa fedha
ili mkakati wao, kwa kutumia umasikini na shinda za Watanzania kwa lengo la
kujinufaisha.

No comments:
Post a Comment