| Mkurugenzi wa wa kampuni ya NPS, Hassan Khan |
UONGOZI inayojishughulisha na uegeshaji wa magari ya Taifa,
National Parking Solution (NPS) imewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuwa
makini na baadhi ya watu wanaotumia vibaya jina la kampuni hiyo na kuwatapeli
wananchi.
Mkurugenzi wa wa kampuni hiyo, Hassan Khan alisema, kumekuwepo na
baadhi ya watu wanaojifanya ni wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuwatapeli
wanananchi pale wanapowakamata kwa kukiuka taratibu za maegesho ya magari.
Alisema tangu kusitishwa na kwa mikataba ya baadhi ya
kampuni zilizokuwa na tenda
na halmashauri za Dar es Salaam ya kukamata watu wanaoegesha magari kimakosa,
kumeibuka watu wanaojifanya kuwa ni watumishi wa kampuni hiyo na kuwatapeli
wananchi.
Khan, alisema pamoja na kujifanya maofisa wa kampuni hiyo, watu
hao huwaomba fedha wananchi wanaowakamata kwa kigezo cha kutowapeleka katika
mamlaka zinazohusika jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa wananchi.
“Kikubwa tunawaomba wananchi wawe makini na ikibidi wawaulize
maswali mengi watu pindi wanapowakamata na uzuri wafanyakazi wetu wote wana
sare maalumu zinazowatambulisha,” alisema Khan.
Aidha, alisema tangu kampuni yake ianze kusimamia shughuli za
uegeshaji magari katika jiji la Dar es Salaam hawajawahi kupokea malalamiko
kuhusu ukiukwaji wa taratibu mbalimbali, jambo ambalo alidai kuwa linawapa
nguvu katika utengdaji kazi wao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki aliziagiza halmashauri zote za mkoa huo kusitisha
mikataba na kampuni za udalali baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa
wananchi .
Alisema, lengo la kufanya hivyo ilikuwa ni kuwaondolea
usumbufu wananchi .
No comments:
Post a Comment