VITENDO vya kikatili vya kupigwa na kunyang’anywa mali za
wafanyabiashara mbalimbali kwa kisingizio cha kusafisha jiji na kugawana badala
ya kupeleka kunakoruhusiwa vimezidi kujitokeza jijini Dar es Salaam.
WAZIRI
Mkuu, Mizengo Pinda aliwahi kuagiza kuwa wakuu wa mikoa na wilaya kukaa na
wafanyabiashara na kuangalia njia nzuri ya kufanya biashara ili kuondoa vurugu
baina yao na
vijana.
Pinda
aliyasema hayo Januaari mwaka huu katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo
kwa Waziri Mkuu alipojibu swali la Mbunge wa Ilala, Iddi Zungu (CCM) aliyetaka
kujua kauli ya Serikali kuhusu polisi na wanamgambo wanaotumia nafasi ya
kusafisha jiji kuwanyanyasa wafanyabiashara na kugawana mali zao.
Amesema
yeye binafsi alitumiwa picha ya watendaji hao wakigawana mali
walizowanyang’anya wafanyabiashara wakiwamo mamalishe, jambo ambalo ni
kuwanyanyasa na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Waziri
Mkuu alikemea kitendo cha watendaji wa jiji na mikoa kutumia kusafisha jiji
kunyanyasa wananchi.
Hivyo
aliagiza wakuu wa wilaya na mikoa kukaa na wafanyabiashara ndogo na kupanga
jinsi ya kuendesha biashara kistaarabu ikiwa ni pamoja na kupanga masoko ya
jioni na Jumapili ili wafanye biashara muda mfupi na kuondoka.
Wakati Pinda akiagiza hayo Jeshi la Polisi wakishirikiana na mgambo
katika mtaa wa Mtaa wa Mkwep na Makunganya jijini jana, walitembeza kipigo kwa
wamachinga kwa madai kuwa walikuwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyo
rasmi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, askari hao wakiwapiga wamachinga hao ambao
walikuwa wakitii sheria kila walipoelekezwa.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema
askari hao waliyokuwa wameshika bastola na bunduki waliwavamia wafanyabiashara
hao na kuanza kukusanya bidhaa zao na kuzipakiza katika gari bila ya
kuziorodhesha kama inavyotakiwa.
Mashuhuda hao walisema baada ya kuona vitendo hivyo vya kikatili
walianza kuwazomea askari hao ndipo akasikika kauli ya mmoja wa askari
akimuelekeza kuwa apige risasi ili kuwanyamazisha wasizomee.
Hata hivyo, askari aliyekuwa akielekezwa alibaki kuhangaika akiwatafuta
watu waliokuwa wakizomea kwani hakuweza kuwaona kwa vile walikuwa wakishuhudia
tukio hilo
wakiwa gorofani.
“Sisi tukio lile lilikuwa halituhusu lakini kilichotukera ni kuona askari
ambaye anategemewa kuwa mlinzi wa amani
leo yeye ndio anakuwa wakwanza kuvunja amani kwa kuwapora wananchi mali zao
tena kwa kutumia vitisho vya silaha na kipigo bila huruma,”alisema mmoja wa
mashuhuda hao.
Mashuhuda hao wametoa rai kwa serikali kuwa makini na vitendo
vinavyofanywa na askari pindi wanapokuwa kazini kwa baadhi yao siyo waaminifu, vitendo hivyo vikiachwa
viendelee uhusiano kati ya raia wao utakuwa mbaya.
Mbunge wa Ilala (CCM), Iddi Zungu, amekuwa mstari wa mbele katika
kupambana na vitendo vya baadhi ya wanamgambo na polisi wanaotumia nafasi zao
vibaya kwa kuwanyasa na kuwanyang’anya mali zao wafanyabiashara na kuzigawana
mali hizo.
No comments:
Post a Comment