KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 16 April 2015

SINGU: NITAPIGANIA MGAO WA RASILIMALI ZA MKOA WA SHINYANGA KWA AJILI YA WANANCHI

NA MWANDISHI WETU

MWANACHAMA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Muhima Singu, ametangazania ya kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini, linaloshikiliwa na Stephen Masele wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Singu, ambaye ni msomi wa Chuo Kuu na mfanyabiashara, alisema kutangaza kwake nia ya kugombea nafasi hiyo kumetokana na nchi kuwa katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Miongoni mwa maandalizi hayo ni pamoja na uboreshaji wa daftari la mpiga kura kwa ktumia mfumo wa kieletriniki (BVR), huku Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakidai Tume huru itakayosimamia uchaguzi huo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Singu, alisema kuwa anawaomba wananchi wa jimbo hilo, kumchagua yeye wakati utakapowadia ilia je kushirikiana nao katika kuleta mapinduzi ya maendeleo ya jimbo hilo ambalo wambunge waliopita wa CCM wameshindwa kufanya hivyo.

Alisema endapo atafanikiwa nia yake hiyo, atahakikisha kuwa mgawo wa mapato yanayotokana na rasilimali zote zilizoko katika mkoa huo zinagawanywa sawa kwa wananchi wote bila kubagua.

“Shinyanga ni mkoa waenye migodi mingi ambapo mingine ni ya miaka mingi lakini inashangaza kuwa mgawo wa mapato yanayotokana na uuzwaji wa madini haujaleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi kwa zaidi ya miaka 50 tangu nchi ijitawale,”alisema Singu.

Alisema wakazi wa jimbo hilo wanakabiliwa na umasikini wa kutisha kwani vijana wengi hawana ajira kutokana na ajira nyingi katika migodi kushikwa na wageni.

“Haya nitayapatia ufumbuzi kwa kuzingatia umakini wa sera bora za chama chetu, ambacho kimejipanga kuwakomboa wananchi kutoka katika lindi la umasikini,”alisema Singu.

Hata hivyo, alisema yapo baadhi ya masuala ya kijamii ambayo yako ndani ya uwezo wake kwa kushirikiana na wananchi atayapatia ufumbuzi.


Aidha, alisema kuwa atashirikiana na taasisi zote za kijamii ikiwemo za dini ambazo ziko karibu zaidi na jamii katika kutoa elimu ya ni muhimu

No comments:

Post a Comment