KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Saturday, 2 May 2015

ISSA: SRIKALI YA ZANZIBAR NI 'FEKI'



MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa,  (Chadema), Hashim Juma Issa, amesema kuwa serikali ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar ni ‘feki’.
Mwenyekiti huyo, amabaye alikuwa mgeni rasmi, alitoa kauli hiyo wakati wa Kongamano la Baraza la Wazee wote wa Chadema wanaoishi katika jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema, hivyo, kwa vile kuna ushahidi unaoonesha kuwa Wazanzibari wote ni Watanzania kutokana na kuwa na vipande vya uraia wa Tanzania ambapo  Rais wake ni Jakaya Kikwete, kitendo hicho kitendo kinadhirisha wazi kuwa Zanzibar haina raia wala serikali yake.
“Ndugu zangu mimi ni mzanzibari tutaitetea Zanzibar kwa nguvu zetu zote simuogopi mtu yeyote muda wa kuogopana umekwisha iliyobaki sasa ni vitendo,”alisema Juma.
Juma, alisema anashangaa kumuona Dk. Muhamed Ali Shein kujidai kuwa ni Rais wa Zanzibar wakati hakuna raia hata mmoja Wazanzibar kwa hiyo alimtaka rais huyo aeleze raia wakwe wako wapi.
“Sasa huna huruma, kama huna raia wewe ni rais wa nani, ile iliyoko Zanzibar ni Serikali feki, Wazanzibari watambue kuwa hawana serikali hawa wanajidanganya,”alisema.
Juma, alisema Tanzania kuna serikali moja wasiwadanganye wananchi, kutokana na mazingira hayo Chadema inataka kuleta mfumo wa serikali tatu, ambazo zitakuwa ni Tanganyika, Zanzibar zote hizo kila moja ikiwa na mamlaka yake.
Alisema, baada ya kuanzishwa serikali hizo kutakuwa na serikali moja ya shirikishoku hivyo kuwa taka wazee kusimamia hilo kwa kutumia hekima zenu.
Kuhusu Wazee, Mwenyekiti huyo, aliwaomba wazee hao wapinge baadhi ya maneno ya wanasiasa kuwa Chadema hivi sasa hakina uwezo wa kutongoza kwa maana ya kutoa rais wa nchi bali hadi mwaka 2020.
Aliema kuanzia sasa wazee watambue kuwa wana jukumu kubwa alikutoa ushauri ambao utakisaidia chama wakati kikielekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Suzan Lymo, alisema kuwa Sera ya Chadema iko wazi kuhusu wazee, kwani kitakapoingia madarakani kitakuwa na utaratibu wa kuwalipa pensheni.
Alisema utaratibu wa serikali ya sasa umekuwa ukibagua katika kuwalipa pensheni wazee kwani wanaolipwa ni wale walikuwa wakifanya kazi katika za umma.
Aidha, aliwataka wazee kuhamasishana katika suaala la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwa vile bila ya kufanya hivyo watakosa fursa ya kupiga kura Oktoba mwaka huu.
“Nawaomba wazee kuanzia sasa msikae kimya huu uwe ni mwanzo mzuri, muwe mnatoa matamko pindi mnapoona mambo yanaharibika hukuchi,’alisema.
Susan, aliongeza kuwa pia wazee hao watumie hekima zao kwa kujiepusha kwa kujiingiza katika migogoro hususan kwa kuwapendelea baadhi ya wanachama wanaotaka kugombea nafasi za uongozi.

No comments:

Post a Comment