KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 15 May 2015

CHADEMA YALIA KUFANYIWA RAFU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA CHALINZE


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinadaiwa kuvunja Sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwashawishi wananchi wa Kijiji cha Mtambani Kata ya Bwiringu, Chalinze mkoani Pwani, kukichagua chama hicho.
Kijiji hicho kinatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa kesho, baada ya ule uliyofanyika Desemba 14 na 21 mwaka jana kukumbwa na dosari lukuki zilizosababisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Akizungumza na wandishi wahabari leo, kwa njia ya simu kutokea katika jimbo hilo la Chalinze jana, Katibu wa Operesheni, Mikakati, Propagandi na Mafunzo Mkoa wa Pwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Mwipopo, alisema wanafuatilia kwa karibu ukiukwaji huo wa sheria.
Aliitaja sheria hiyo kuwa ni ile ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji sura namba 287 kifungu cha 201(A), tangazo la serikali namba 320 la 5/9/2014 pamoja kifungu cha 18.
Mwipopo, alisema kifungu hicho cha 18 kinaeleze masharti ya mgombea au chama kutojihusisha na kampeni zinazoashilia vitendo vya rushwa, kashfa, matusi, ubaguzi wa kijinsia, udini na ukabila.
Alisema pamoja na sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa wazi, Mei 11 mwaka huu CCM kilizindua kampeni zake, ambapo walitoa fulana, jezi na mipira katika shule na wananchi ikiwa ni kuwashawishi ili waweze kukichagua chama hicho kwenye uchaguzi huo.
“Pia waliendelea kuvunja kanuni hizo kwa kuwaambia wananchi wa kijiji cha mtambani kwamba wakikichagua Chadema watawafukuza wafugaji wote, niwaombe wafugaji kuzipuuza kauli hizo kwani Chadema ni chama makini ambacho kazi yake kubwa ni kupigania haki za wananchi wote bila ya kubagua popote pale nchini,”alisema Mwipopo.
Alisema Chadema siyo chama cha kibaguzi wala kikabila bali ni chama cha wananchi kutoka maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano, hivyo wanaokifananisha na udini na ukabila ni watu waliofilisika kisiasa.
Katibu huyo, alisema kuwa wananchi wa Mtambani hawahitaji fulana, mpira bali wanahitaji barabara, maji na huduma bora za afya, ambazo CCM, imeshindwa kuwafikishia tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1964.

No comments:

Post a Comment