MWENYEKITI wa Bodi ya
Mamlaka ya Manunuziya Umma (PPRA), Dk. Matern Lumbanga, ameshangazwa na baadhi
ya mawaziri wanaosema kuwa Sheria ya manunuzi ni mbaya wakati wameipitisha
wenyewe bungeni.
Ikumbukwe manunuzi ya umma
huchukua takriban nusu ya fedha za bajeti yote ya serikali, hivyo usimamizi
mzuri katika sekta hiyo unahitaji mchngo wa wadau wote ili kuhakikisha
upatikanaji wa thamani bora ya fedha za umma.
Kauli hiyo aliitoa jijini
Dar es Salaama jana wakati alipozungumza na wandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya PPRA kutimiza miaka 10 tangu ilipoanzishwa mwaka 2005.
Dk. Lumbanga, alisema wote
wanaolalamikia Sheria hiyo na kudai kuwa ni mbaya, inatikana sheria hiyo kuwanyima
kufanya vitendo vyao vya kifisadi katika fedha za umma.
Aliongeza kwa kusema kuwa
kuna baadhi ya idara za serikali zimekuwa zikienda kinyume na sheria hiyo, kwa
kutoa zabuni bila ya kuzitangaza.
“Kazi ya Sheria hiyo ni kusimamia
na kudhibiti manunuzi ya umma yasiweze kutumika kinyume na sheria,”alisema Dk.
Lumbanga.
Alisema, serikali
ikifanikiwa kudhibiti manunuzi nje ya sheria hiyo, basin chi kupiga hatua
kimaendeleo na kupunguza umasikini.
Aidha, alisema inapobainika
kunawaliofanya manunuzi kinyume cha sheria hiyo, PPRA haiwaachi na kwamba
inawachukulia hatua za kisheria.
Akizungumzia maadhimisho
hayo, Dk Lumbanga, alisema yatafanyika siku tatu kuanzia Mei 18 hadi 21 mwaka
huu ambapo yatazinduliwa na Waziri waziri wa Fedha na Uchumi Saada Mkuya,
atayazindua Mei 19 mwaka huu, yatafanyika katika ukumbi wa Dimond Jubilee.
Alisema, lengo maadhimisho
hayo ni kuwakutanisha wadau wa manunuzi ya umma nchini kujadili mafanikio
yaliyopatikana katika sekta ya hiyo muhimu hususan katika kipindi hicho cha
muongo mmoja wa uwepo wa mfumo imara wa usimamizi na udhibiti manunuzi.
Aidha, wadau watapata fursa
ya kujadili matatizo mbalimbali ambayo wanakabiliana nayo katika sekta hiyo na
kupendekeza mikakati yenye lengo la kuboresha zaidi.
Dk. Lumbanga alisema
maadhimisho hayo yataanza kwa wasrsha maalum ya wadau wa habari hususan wandishi
habari kutoka mikoa mikoa yote nchini, wahariri, wakilishi kutoka Baraza la
Habari Tanzania (MCT) na Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC).
“Warsha hiyo itafanyika Mei
18 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee,”alisema Dk. Lumbanga.
Dk. Lumbanga, ametoa wito
kwa wadau wote wa manunuzi nchini na umma kwa ujumla kujitokeza kushiriki
kwenye maadhimisho hayo.

No comments:
Post a Comment