KIKOSI cha Usalama Barabarani
nchini, kimetangaza rasmi kutokuepo kwa mafunzo ya madereva wote
wanaoendesha vyombo vya moto wala kutakiwa kwenda kusoma kwa mwaka huu.
Hivi karibuni
serikali ilipitisha sheria ya
barabarani ya mwaka 1977 ambayo iliboreshwa,
ikiwataka madereva kwenda kusoma pamoja na gharama ya mafunzo
kutakiwa kulipa ada ya sh.560,000.
Sheria hiyo pia
iliwataka madereva wa magari mengine
kuchunguzwa afya zao na kujaribiwa kila baada ya miaka sita.(The Road Traffic
Examination ana Re-Testing of Drivers)
Regulation GN No 31 ya januari 30 mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda
wa kikosi hicho, Mohammed Mpinga, alisema Sheria hiyo ilisababisha
madereva hao kugoma kusafirisha abiria
na mizigo hali iliyosababisha adha kubwa kwa wananchi pamoja na kuathiri uchumi
wanchi.
Mpinga, alisema hayo kwa vile
mitaala ya mafunzo hayo mafupi haijakamilika na shule zitakazohusika
hazijaanishwa pia ada za mafunzo
hazijapangwa.
Alisema, kuwa
ada ya sh 560,000 iliyotangazwa hivi karibuni haijawahi kutamkwa na
serikali bali ilitamkwa kienyeji na Mkuu wa chuo cha Taifa cha
usafirishaji(NIT), Dk. Zakaria Mganilwa.
Mpinga, lisema serikali
imesitisha sheria ya kwenda kusoma kwa mwaka huu na kudai kuwa itakamilishwa mwaka ujao wa bajeti 2016 hadi
2017 ambapo mpaka kufikia hapo madai ya
madereva hao watakuwa wamekamilishwa na kuboreshewa.
Aliongeza kuwa kwa madereva ambao leseni zao zimekwisha au
zitaisha katika kipindi hiki watabadilishiwa na kuhusisha leseni zao kwa
utaratibu wa zamani bila kuulizwa vyeti vya mafunzo mafupi (Refresher
course).na kuwataka watakao ulizwa watoe taarifa.
“Nawataka madereva wote wawe
na uvumilivu kwa matatizona changamoto zao kwani kamati ya Kudumu ya kutatua
matatizo katika sekta ya usafirishaji iliyoundwa na waziri mkuu itayapatia
ufumbuzi wa kudumu”alisema Mpinga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
madereva nchini, Clement Masanja, alisema Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, ilipewa taarifa kuwa sheria
ya kuwataka madereva kwenda kusoma mwaka huu imefutwa.
“Kuanzia sasa hakuna dereva
atakayeulizwa habari ya cheti, imeundwa tume ambayo imeshaanza kazi hakuna kusoma ila madereva wafuate
sheria za barabarani, nawatakia madereva wote wafanye kazi kwa amani na utulivu kwani haki zao zimeanza
kuboreshwa.”alisema
Masanja.
No comments:
Post a Comment