RAIS Mstaafu
Benjamini Mkapa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Bodi ya
Wakandarasi unaotarajiwa kufanyika Mei 14 hadi 15 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Akitoa
taarifa hiyo katika Ofisi ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mwenyekiti wa
Maandalizi ya Bodi hiyo Mhandisi Dk Mwakyusa Ambwene, alisema kwa kawaida
mkutano huo utawahusisha wadau wote wa sekta ya ujenzi.
Alisema siku
hiyo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazoanywa ikiwa ni pamoja na
majadiliano ya kitaaluma, kiapo cha wahandisi wataalamu.
Dk. alisema
pia kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya kiufundi na biashara vifaa
vinavyohusiana na ujenzi.
Naye,
Msajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Jehad Abdallah
Jehad, amezitaka Taasisi, Mashirika na wafanyabiashara mbalimbali kutumia fursa
hiyo kuonyesha bidhaa zao katika mkutano huo wa mbili ili kudhihirishia umma
juu ya kazi wanazozifanya kwa maendeleo ya nchi.
Aliongeza
kuwa mkutano huo una lengo la kuwatia moyo wanafunzi wa kitanzania wanaosomea
uhandisi ili wafanye vizuri zaidi katika masomo yao na kuwafanya vijana washawishike kusomea
taaluma hiyo.

No comments:
Post a Comment