![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu aliyemaliza muda wake Elizabeth |
SHIRIKA
la HakiElimu litaendeleza harakati zake za kuwapatia taarifa mbalimbali wananchi ili waweze kushiriki katika kuchangia mwazo ambayo yatasaidia kuboresha elimu na
demokrasia kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Taifa.
John Kalage (JK), alitoa kauli hiyo wakati wa hafla fupi
ya kumuaga Elizabeth Missokia ambaye alikuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo kwa pindi cha miaka saba na
kumkaribisha mkurugenzi mpya ambaye ni Kalage.
Mkurugenzi
huyo mpya, alisema kuwa anaamini elimu bora inasidia, inakuza usawa, ubunifu,
udadisi, na demokrasia kwa ujumla.
“Harakati za wadau wa elimu ni mojawapo ya nyenzo
zinazotumika kuhamasisha ushiriki huu wa wananchi na hizi ni harakati za
wananchi, mashirika na taasisi zenye nia ya kuongeza kasi ya kuleta mabadiliko
chanya katika elimu na demokrasia nchini,”alisema JK.Aidha, Kalage ameahidi kutekeleza kwa vitendo yale yote
yaliyoanzishwa na mtangulizi wake ikiwemo kuanzishwa shule itakayo kuwa mfano
wa elimu bora, inayotakiwa kutolewa katika shule zote nchini.
Elizabeth, wakati akiwaaga wafanyakazi wenzake, alisema kufanya
kazi katika shirika hilo kunataka wakati mwingine kuwa na kichwa cha
mwendawazimu.Alisema hivyo kutokana na baadhi ya watendaji waserikali
kulichukulia shirika hilo kama vile linawapotosha wananchi kuhusu atua
mbalimbali zinazotekelezwaa na serikali.
“Shirika halina nia mbaya na linaamini yapo mengi mazuri
yaliyofanywa na kila wanachokikosoa lengo lake ni kuwatakiwa watoto wa wote wa
Tanzania wapate elimu ambayo itawaokoa ‘na ufaulu wa ‘zero’,”alisema Elizabeth.Elizabeth, aliwaasa wafanyakazi wezake waliobaki kuwa wasikate
tamaa bali waongeze kasi katika mapambano yao ya kuleta mapinduzi
yatakayosaidia watoto wa kitanzania kupata elimu bora na siyo bora elimu.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji cha Miradi ya Matokeo
Makubwa sasa (BRN), kutoka Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Grace Hoka, alisema serikali inatambua kazi nzuri ya
shirika hilo na iko tayari kushirikiana nalo kinyume na baadhi ya wadau wanavyo
dhani.

No comments:
Post a Comment