![]() |
| Badhi ya Watendaji wa TAWLA wakiwa na Mkurugenzi Mtendaji, Tike Mwambipile, aliyevaa kofia |
ZAIDI ya watu milioni 15 wenye matatizo ya kisheria wamepata msaada wa huo kupitia Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), tangu kilipoanzishwa miaka 25 iliyopita.
Hayo yalisemwa leo,
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile wakati alipozungumza na wandishi
wa habari kuhusu ratiba ya maadhimisho ya sherehe za chama hicho, kutimiza miaka
hiyo, ambapo pia watatoa elipmu kuhusu masuala ya sheria.
Alisema pamoja na kutoa
msaada huo wa kisheria, pia wameweza kuihamasisha jamii juu ya masuala ya
kisheria kupitia machapisho mbalimbali, mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria.
“Pia tumeweza kuwafikia kwa
kupitia vyombo vya habari, michezo ya kuigiza vyote hivyo vivilikuwa vichocheo
ambavyo vimetufanya tuwafikie watu hao milioni 15,”alisema Tike.
Akizungumzia ratiba ya
sherehe hizo, alisema kuwa zilianza jana hadi Mei 30 kutakuwa na mwendelezo wa
vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu masuala ya sheria na haki za binadamu
kupitia vyombo vya habari katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma,Tanga na Arusha.
Aliongeza kuwa katika
maadhimisho hayo Mei 29 mwaka huu kutakuwa na matembezi kutoka Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu hadi Karimjee na kupokelewa na Rais Jakaya Kikwete.
Tike alisema siku
inayofuata kutakuwa na Mkutano Mkuu wa wanachama na jioni ambao utazungumzia
mizungumzia mipango ya baadae ikiwa ni jinsi gani chama hicho kitafanyakazi
katika mikoa yote nchini.

No comments:
Post a Comment