KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 13 May 2015

MHITIMU WA CHUO CHA KODI KYARUZI ATANGAZA NIA

MHITIMU wa masuala Kodi na Forodha katika Chuo cha Kodi, Franklydommy Kyaruzi, ametangaza nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kugombea  udiwani Kata ya Kimanga wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Kata hiyo, hivi sasa inashikiliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema).
Hata hivyo, ili apate nafasi hiyo atahitaji kwanza  ridhaa ya chama chake baada ya kufanyika kura za ndani.Akizungumza na mwandishi wa Sauti Pevu jijini juzi, Kyaruzi, alisema, akifanikiwa katika harakati zake hizo anatarajia kutumia sera zake ujana zaidi.
“Sera zangu ni tofauti kwa vile naamini diwani aliyopo ametekeleza ahadi zake kwa sehemu yake hivyo, ninachotaka ni kumpokea, ukichukulia kuwa mimi ni kijana nataka kutumia sera zangu za ujana,”alisema Kyaruzi.
Alisema msukumo wa kugombea nafasi hiyo umetokana na kubaini kwake matatizo yanayowakabili wakazi wa kata hiyo.
Aliyataja, matatizo hayo kuwa ni eneo hilo kugeuzwa kuwa kambi ya watumiaji wa dawa za kulevya (Mateja), uchafu uliyokithiri na vijana kutopenda kufanyakazi.
Aidha, ili yote hayo yafanikiwe, anapaswa kujenga umoja na ushirikiano kitu ambacho hivi sasa kinakosekana katika kata hiyo.
“Kwa Kata ya Kimanga nasubiri tu uwamuzi wa ndani wa chama changu lakini kwa upande wa wakazi wenzangu wananiamini bila shaka najiamnini kwa hilo,”alisema Kyaruzi.
MWISHO

No comments:

Post a Comment