Meneja
Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi
Simon Jilima (kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi
kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani
ni Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg, Robert Masatu na Ndg. Aloce
Shayo, kwa mfuatano.
Meneja
Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi
Jilima akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya
Mipango, Bibi. Florence Mwanri, eneo likatalojengwa kituo cha Kinyerezi
II mara baada ya Kinyerezi I kukamilika.
Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi.
Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi kwa juu.
…………………………………………………………..
Kituo cha kuchakata na kuzalisha
umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na
kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa
Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon
Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi
kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.
“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni
ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo
wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la
viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.
Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongolamboto.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya
Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu
utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni
dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa
zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Katika miaka mitano ijayo mpango
wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni
vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika
utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” alisisitiza
Bibi. Mwanri.
Ili kuongeza uzalishaji wa nishati
hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha
umeme kiasi cha kV 180.
No comments:
Post a Comment