KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 21 May 2015

KIPINDUPINDU CHA TISHIA UHAI WA WAKIMBIZI WA BURUNDI

 Baadhi ya wakimbizi wakiwa wamewasili Kigoma
 Wakimbizi kutoka Burundi wakisubiri huduma mbalimbali za kijamii.
 Mmoja wa wakimbizi akiwa anapata matibabu.
 Hapa watoto wa wakimbizi wakijipikia Chakula , katika mazingira hatarishi.
 Mamia ya wakimbizi wakiwa wanatafakari hatima yao.
 Hii ndio hali halisi ya vyoo ambavyo vimechangia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.Wafanyakazi wa Shirika la Oxfam wakishusha vifaa kwa ajili ya vifaa vya upatikanaji wa maji na vyoo ili kubabiliana na Kipindupindu. 
 Hiki ni moja ya chanzo cha maji.
 Wakimbizi wakiwa ndani ya Meli.
………………………………………………………………………….
ONGEZEKO la wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi pamoja na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo maji safi linamaanisha 
kuongezeka kwa hatari ya mlipuko wa magonjwa ya kuambukizwa hasa kwa 
wakimbizi takribani 40,000 walioko Kagunga mpakani mwa Tanzania. 
Tayari 
watu 20 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo 
ya Kagunga na katika kambi ya Nyarugusu ambapo wakimbizi hupelekwa kwa 
ajili ya makazi.
Shirika
la Umoja wa Mataifa (UN) limeripoti uwepo wa watu 1057 wenye dalili za 
kuharisha waliopo Kagunga ambapo wakimbizi husubiria usafiri wa boti 
zinazowasafirisha kwenda Kigoma. 
Kuna
uhitaji wa haraka sana wa huduma za msingi ikiwemo maji safi na vyoo.
Shirika la Oxfam linafanya kazi na shirika la TWESA ili kutoa ufumbuzi 
wa haraka kukidhi mahitaji hayo kwani kuna uhitaji wa haraka sana wa 
maji safi, huduma za matibabu pamoja na vyoo. 
Shirika 
la Oxfam tayari limeanza maandalizi ya haraka ili kuongeza upatikanaji 
wa maji safi na kujenga vyoo vya dharura katika kambi ya Nyarugusu ili 
kukabiliana na ongezeko kubwa la wakimbizi. 
Inakadiriwa 
takribani wakimbizi 22,000 wamesafirishwa kutoka Kagunga kwenda katika 
kambi ya Nyarugusu ambapo wanapewa makazi ya muda mfupi katika shule na 
makanisa wakati mashirika mbalimbali ya misaada yakiendelea kutoa vifaa 
vya ujenzi wa makazi ya muda mrefu. 
Huduma za matibabu katika makambi ya wakimbizi zinasua sua kutokana na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa mbalimbali.
Uhitaji wa haraka wa huduma za msingi ni muhimu ili kuzuia ongezeko la magonjwa yanayosambaa kama kipindupindu. 

No comments:

Post a Comment