KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 21 May 2015

KISARAWE YATOA FURSA KWA WAWEKEZAJI

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kisarawe, mkoani Pwani imetangaza viwanja 291 kwa ajili ya fursa za uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje kuanzia sasa.
Fursa hiyo inakuja baada ya wilaya hiyo kuanzisha Mradi wa Uendelezaji wa Ardhi, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kisarawe katika kipindi cha mwaka 2013/14.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani hapa, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mwanvua Mrindoko, alisema viwanja hivyo viko katika maeneo ambayo hayana migogoro.
Mrindoko alisema eneo hilo ambalo linafaa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda linapatikana katika Kijiji cha Visegese, kilomita nne kutoka mji mdogo wa Kisarawe.
“Katika eneo hili kuna njia mbili za reli ambazo zinapita karibu kabisa na eneo hili la uwekezaji, pia haliko mbali na Barabara ya Morogoro.
“Nawaomba kila anayehitaji kuwekeza anakaribishwa Kisarawe kwani fursa zote ikiwemo ubora wa miondombinu vinapatikana kirahisi,” alisema Mrindoko.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Adam Ng’imba, aliwatahadharisha wananchi na kuwataka watambue kuwa ardhi isiyopimwa na kumilikishwa inakosa thamani halisi na kushindwa kumtajirisha mmiliki wake.

k2 k3 k5 k6Baadhi ya madiwani na wanakamati wa mradi huo wakiwa kwenye mkutano huo.k7 (2)
Mkutano huo ukiendelea

K8
Kitabu kinachouelezea mradi huo

No comments:

Post a Comment