KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 18 May 2015

MJUE MBUNIFU WA JINA LA TANZANIA


MWANDISHI wa mtandao huu Alphonce Tonny Kapelah kutoka Mtwara ameona aufahamishe umma juu ya mwasisi wa jina la Tanzania.
Mwandishi aliandika makala haya wakati ilipotimiaka 50 ya Uhuru wa Tangayika, najua wengi wetu hatujui historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar maana tuliwakuta waasisi wetu wameishafanya zoezi hilo,tusilijadili sana kwa kuwa lengo lao lilikuwa zuri.
Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la Tanzania pata historia ya namna alivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A
Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kukutana na huyo ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania.
Imekuwa kama Bahati nimekutana na Mtu huyu aliyebuni jina la Tanzania Mkoani Mtwara,sehemu ambayo tayari naiweka kwenye Historia yangu hata kesho nikiondoka Mtwara nitaikumbuka Radio yangu Safari Radio.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944,Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T  A DAR  alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGAKAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya Hapo alikuja baadae kujiunga na Chuo cha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza  jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar,Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard siku hizi Daily News akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar
Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano,Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika.
Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapata TANZAN alivyoona hivyo akachukua  I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukua A kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na A kwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA.
 mfano EthiopIA,ZambIA,NigerIA,TunisIA,SomalIA,GambIA,NamibIA,LiberIA,MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika,Zanzibar,Iqbal na Ahmadiyya
Mohammed Iqbal  Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu  Shindano
Baada ya Muda mwingi kupita  baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea Barua nzito kutoka serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo…

No comments:

Post a Comment