KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 18 May 2015



SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
(TANESCO)



TAARIFA YA KUREJEA KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA HUDUMA YA LUKU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wote wanaonunua umeme wa LUKU kwa njia ya mitandao kwamba, huduma hiyo kwa sasa imerejea kwenye hali ya kawaida.


Itakumbukwa kwamba kulitokea usumbufu kwa wateja wetu kushindwa kununua umeme wa LUKU baada ya TANESCO kusitisha huduma kwa mmoja wa Mawakala wake Aprili 28, 2015.

Tunapenda kuwahakikishia na kuwaondoa hofu wateja wetu wote kwamba mfumo wa LUKU wa Tanesco upo salama na waendelee kununua umeme kupitia mitandao na mawakala wetu kama kawaida.

Shirika linawaomba wateja wote wenye matatizo ya kutopata “Units” baada ya kutuma pesa zao au “Units” kushindwa kuingia kwenye mita, wawasiliane na Ofisi yoyote ya Tanesco iliyokaribu.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika kipindi hicho.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment