![]() |
| Mwenyekiti wa NEC, Lubuva |
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza kumaliza kazi ya ugawajiwa majimbo mapya Juni mwishoni kwa ajili ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Akitangaza uamuzi huo Dar es Salaam jana mbele ya viongozi wa vyamavya siasa, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Kombwey alisema kuwaugawaji huo utaanza leo.“Tunaanza leo kupokea mapendekezo kutoka katika mikoa mbalimbali, kwaajili ya kuyafanyia kazi na kuyatolea uamuzi yale yatakayokuwa na sifakugawanywa Juni mwishoni,” alisema.Mkurugenzi Kombwey alisema kuwa mwisho wa ukamilishwaji wa upokeaji wamaombi ya majimbo mapya unatarajiwa kufanyika Mei 31, mwaka huu.Kombwey aliyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Mwenyekiti NEC,Jaji Mstaafu Damian Lubuva kuelezea ugawaji wa majimbo mapya yauchaguzi yatakayozingatia vigezo 13 ikiwa ni pamoja na jimbo kuwandani ya halmashauri au wilaya mbili hali inayomfanya mbunge mmojakutumika katika sehemu hizo mbili.Mchakato huo wa kugawa majimbo ya uchaguzi ulianza jana kwa tume kutoatangazo katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi. Jaji Lubuva alitaja taratibu zinatarajiwa kutumika kuwa ni pamoja namgawanyo wa wastani wa idadi ya watu ambayo itapatikana kwakuzingatia idadi ya watu wote nchini, wa mijini na vijijini. Alisema kigezo kingine kitakachotazamwa ni idadi ya watu itakayotokanana makisio ya ongezeko la watu hadi kufikia Julai mwaka huu na kwakuzingatia Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.“Pia kigezo chetu kingine ni upatikanaji wa mawasilianoyanayomuwezesha mwakilishi kuwafikia kwa urahisi wananchi kwa njia yasimu, barabara, vyombo vya habari.“Pia tutaangalia jografia kwa kuangalia mahali iwapo jimbo litakuwamilimani, visiwani au mabondeni ili kujua namna bora ya uwasilishwaji wake,”
Alisema katika ugawaji wa majimbo mpya pia itaangaliwa hali ya uchumi ikiwa na dhamira ya kukwepa maeneo yenye uchumi mkubwa kumeza katika uwakilishi maeneo yaliyo chini katika uchumi.
“Takwimu zitakazotumiwa ni za ukusanyaji wa mapato zilizopatikanakutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), asilimia ya watu walio chini ya kiwango cha umasikini kilichopatikana katika Ofisi ya Makamu wa Rais(OMR),” alisema.
Alisema ukubwa wa jimbo husika na taarifa zake zitakazopatikana
katika OMR na NEC, ni miongoni mwa vigezo vitakavyotumika katika kupata majimbo mapya ya uchaguzi.
“Mipaka ya utawala na pale ambako itabadilika kabla ya kufanya ugawaji wa majimbo, NEC itazingatia mabadiliko hayo. Uwepo wa kata moja kutokuwa katika majimbo mawili na kuangalia mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo, ikiwamo mazingira ya muungano. “Tanzania ni muungano wa nchi mbili hivyo ugawaji wa majimbo
utazingatia upekee wa mazingira ya Muungano,” alisema.
Jaji Lubuva alisema kigezo kingine kitakachoangaliwa ni uwezo wa
ukubwa wa Bunge kuepuka kuzidisha idadi tofauti na inayostahili.
Vigezo viti maalumu Mwenyekiti huyo NEC alisema kigezo kingine ni kuhusu viti maalum vya wanawake ambako kwa mujibu wa Katiba imetengwa asilimia 30 ni kwa ajili ya wajumbe wanawake ili kuweka usawa wa jinsia. “Kutokana na ukweli kwamba idadi ya wanawake wa viti maalumu imekuwa ikiongezeka kila mwaka wa uchaguzi, hivyo kama mwaka huu itaongezeka, NEC itabidi izingatie ongezeko hilo,” alisema.
Majimbo mapya kutokana na hali hiyo baadhi ya majimbo ambayo yanaweza kugawanywa ni pamoja na jimbo la Kahama Mjini ambalo lipo katika halmashauri mbili za Ushetu na Kahama, hali inayomfanya mbunge wa sasa kuhudhuria vikao katika maeneo yote mawili.
Majimbo ya Kondoa Kusini na Kaskazini nayo yanatarajiwa kuingia katika kugawanywa baada ya Wilaya ya Kondoa kugawanywa na kuzaliwa wilaya mpya ya Chemba.
Pia majimbo ya Mbinga Mashariki na Magharibi nayo huenda yakaingia katika vigezo vya NEC baada ya kuanzishwa kwa Wilaya mpya ya Nyasa. Majimbo ya mwaka 2010
Mwaka 2010, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iligawa majimbo mapya ambayo ni Tunduru (Ruvuma) yalizaliwa majimbo ya Tunduru Kaskazini naKusini, Nkasi (Rukwa) yalianzishwa majimbo ya Nkasi Kusini na Kaskazini, Maswa (Simiyu) Maswa Magharibi na Mashariki, Bukombe(Shinyanga), Singida Kusini (Singida), Kasulu Mjini na Vijijnini(Kigoma) na Ukonga na Segerea (Dar es Salaam).
Uamuzi kuhusu mapendekezo ya kugawa majimbo ya uchaguzi ulifikiwa naNEC baada ya kufanya uchambuzi.
Mapendekezo hayo yaliwasilishwa NEC na Kamati za Ushauri wa Mkoa (RCC)baada ya halmashauri 45 kupeleka maombi 47 zikitaka kugawanywamajimbo yao.
Hofu kwa wabunge kutokana na taarifa za ugawaji wa majimbo hivi sasa idadi kubwaya wabunge wamejichimbia majimboni kusubiri hatima yao.

No comments:
Post a Comment