RAS Jakaya Kikwete, amemteua Kamishna wa Polisi (CP), Diwani Msuya,
kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyosainiwa na Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi Ikulu, Premi Kibanga, kabla ya uteuzi huu CP Msuya,
alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Kamishna Msuya anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na Robert Manumba, ambaye amestaafu
kwa mujibu wa Sheria.
Aidha, Rais Kikwete, pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP),
Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi iliyoachwa
na Kamishna Msuya.
Kabla ya uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mwanza.
Uteuzi huu umeanza tarehe Mei 3 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment