MBUNGE wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM), amesema kuwa hana muda wa
kulumbana na wanasiasa wanaosaka tonge kwa kutumia jina lake katika Wilaya ya Ilala.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Zungu alisema, baadhi ya watu
wasiomtakia mema wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii hata kuchapisha
vijarida vya magazeti kwa lengo la kumchafua
mbele ya wapigakura wake.
Zungu alisema kuwa hivi sasa amejikita katika kusimamia na kutekeleza
ilani ya uchaguzi wa CCM na sio kulumbana na watu wanaotafuta ubunge kwa
kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo facebook.
“Unajua kuna mambo yanastaabisha sana kuna watu ambao ni wasakatonge
wanahaha usiku na mchana eti wamchafue Zungu mara amekula fedha za Mfuko wa
jimbo sh. milioni 400 tena hiki kijarida hicho kilika mwaka 2012 na sasa wamerudi
tena,” alisema.
Alisema kuwa jimbo hilo haliwezi kupata kiasi hicho cha fedha kwa
kuwa lina idadi ndogo ya watu huku kamati maalum inayoongozwa na mbunge ndiyo
inahusika na fedha hiyo.
Zungu alisema
wanasiasa wanaolitaka jimbo hilo hawapaswi kuwa na hofu kwa kuwa muda ukifika
wanatakiwa kujitokeza ili wakutane uwanjani kwa kuwa waamuzi ni wapigakura

No comments:
Post a Comment