MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda, amesema Tanzania
haina tatizo la ajira ila kuna tatizo la fikra.
Kauli hiyo inakuja baada ya
baadhi ya watia nia wanaomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM),
katika kugombea nafasi ya uraisi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba
mwaka huu, kueleeleza kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni sawa na bomu
linalosubiri kulipuka.
Makonda alitoa kauli hiyo, mwishoni
mwa wiki wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya tano ya Tanzania Homes Expo
yaliyoandaliwa na Kampuni za EAGgroup
jijini Dar es Salaam .
Alisema Tanzania ina
rasilimali nyingi lakini vijana wamekuwa hawazioni fursa ambazo zingeweza
kuwapatia ajira na kuondokana na
kuilaumu Serikali.
“Tanzania ina rasilimali
nyingi ambazo kama vijana
wangezitumia zingeweza kuwapatia ajira na kuondokana
kukimbilia nchi jirani kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya na
kuishia kutofikia malengo yao.”alisema Makonda.
Alisema fursa hizo zimekuwa
zikichangamkiwa na wageni ambao wanatengeneza malighafi kwa kutumia rasilimali
za hapa nchini.
“Vijana wengi wanakimbilia
nje ya nchi wanaziacha fursa na kushindwa
kukuza uchumi wa nchi” alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa Kampuni za EAGgroup, Imani Kajula, alisema maonyesho ya Tanzania
Homes Expo lengo lake ni kutoa elimu kwa jamii ili ielewe usuluhisho mbalimbali wa makazi yao .
Kajura aliongeza kuwa lengo
kubwa la Tanzania Homes Expo ni kuweka jukwaa moja la mtu anayetafuta
usuluhisho wa nyumba kuanzia Ulinzi na kudai kuwa Watanzania wengi hawajui njia za
kuweka maeneo yao
ya makazi yakawa katika hali ya usalama
“Jinsi Nchi yetu inavyozidi
kukua, kunahitajika watoa huduma mbalimbali kwa sababu kumekuwa na ongezeko la
watu wanaohitaji huduma mbalimbali za
makazi yao .
makazi tukaona ni muhimu kuwa na sehemu ambayo watoa huduma na wahitaji huduma
wanakutana kwa pamoja.
Maonyesho haya yanashirikisha
washauri wa masuala ya ujenzi, wajenzi wa majengo na nyumba za kuuza, kampuni
za bima, wanaoendeleza viwanja, Kampuni za fedha pia suala la Afya lipo.”alisema
No comments:
Post a Comment