KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 1 June 2015

MKURUGENZI KINONDONI: WATAKAOBAINIKA NITAWACHUKULIA HATUA



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni, Mussa Natty
MKURUGENZI wa Manispaa ya Kinondoni, Mussa Natty, amesema atawachukulia hatua watendaji wa Idara ya Ardhi watakaobainika kuwa wametoa eneo la barabara ya mtaa wa Uzuri Kata ya Manzese, kwa mfanyabiashara aliyejenga ukuta ambao umesababisha kero kwa wananchi.  
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Natty, alisema kwa vile suala hilo ndio amelipokea hivyo hawezi kulitolea majibu ya haraka. 
Alisema, anatarajia kufanya hivyo baada ya kukutana, watendaji hao, kupata taarifa kisha kuzifanyia uchunguzi kwa ajili ya kubaini kama kweli wapo waliofanya makosa hayo ndipo wachukuliwe hatua za kisheria.“Taarifa hii naichukua kama vile nimepewa na raia na msamalia mwema na kwa kuwa ni wajibu wangu nitaifanyia kazi haraka, nikikata simu tu namuita Mtendaji, aje hapa alete taarifa kuhusu madai hayo,”alisema Natty.Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Jonas Halimoja, alisema mfanyabiashara huyo hatambuliki katika ofisi ya mtaa kwa sababu eneo alilojenga halina vibali vya mtaa ikiwemo fomu maalum ambayo ingemuwezesha kupata leseni ya makazi.“Mimi na wakazi wa mtaa huu tumeshangaa kumuona mfanyabiashara huyu akivamia barabara hii pamoja kuziba, mitaro ya maji, kufunika mabomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasco), tena huku akiwa hana leseni ya makazi ya mtaa huo jambo ambalo limenishtua,”alisema Halimoja.  
Awali wakazi wa Mtaa huo, kwa nyakati tofauti walisema tangu kuzibwa kwa barabara hiyo kumewasabishia kero kubwa ikiwa ni pamoja na kukwama shughuli zote za kijamii katika mtaa huo.“Hatuwezi kuingiza magari kwa ajili ya kuja kubeba maiti kwenda kuzika, wagonjwa kwenda hospitali na kibaya zaidi mvua zilizopita tulitaabika kwa mafuriko kutokana na kuzibwa mitaro huu ni unyanyasaji,”alisekika mmoja wakazi hao.Walisema pamoja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo kuwasihi kuwa wavute subira wakati mgogoro huo unashughulikiwa, wanaamini kuwa iko siku wataubomoa kwa nguvu.Aidha, walisema ili wasifikie hatua hiyo wanamuomba Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Williamu Lukuvi, atambue kilio chao hicho.

No comments:

Post a Comment