MBUNGE wa Pangani Tanga, Salehe Pamba, anakabiliwa na upinzani mkali katika kutetea
jimbo hilo kutokana na kujitokeza wanachama wenzake nane wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), kuwani kuteuliwa na chama hicho ili kupeperusha bendera ya chama hicho
katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Wakati wakichukua fomu, wanachama hao kila mmoja alisema
kuwa amesukumwa na nia ya kutaka kupigania matatizo ya wananchi.
Akizungumza kwa njia simu kutokea Pangani jana, John Semkhande, ambaye ni diwani anayemaliza
muda wake katika kata moja wilayani humo, alisema msimu huu CCM inategemea
kupata wagombea wengi zaidi ya hao.
Aliwataja wanachama hao waliojitokeza kuwa ni Salehe Pamba
ambaye ndiye mbunge wa sasa, Rosemery Alfred, Juma Aweso, Ayoub Mswahili na
Halima Kimbau.
Wwngine ni Rished Mohamed ambaye aliwahi kuwa mbunge kwa
kipindi cha miaka 15, Abrahaman Magati, Omary Chanbega na Elzabeth Alatanga.
Akizungumzia kujitokeza kwa wanachama wengi kinyume na
miaka awali, Senkhande, alisema hiyo ni kuonesha ni jinsi gani wanachama hao
walivyoshikwa na hamu ya kuwasogezea maendeleo wananchi.
“Unajua mimi kwa taaluma ni mwandishi wa habari na
mwanachama wa CCM, lakini kujitokeza kwa wanachama hao katika kuwania nafasi
hiyo, huenda kuna mambo wameona hayakwenda sawa au ni utaratibu tu, kwami
uongozi ni sawa na mbio za kijiti na inafikia wakati lazima alyoko madarakani amkabidhikijiti kwa mwingine,”alisema
Semkhande.
No comments:
Post a Comment