BAADHI ya Wanavyuo wanomuunga mkono Mbunge wa Monduli
Edward Lowassa (Timu Lowassa), wamejiunga
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kutoridhishwa
na mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama hicho.
Walisema hivyo,
baada ya kubaini kuwa kukatwa kwa jina la kada huyo ilikuwa ni mipango iliyopangwa
kwa lengo la kuwanufaisha watu wengine.
Wakati wakipokea kadi za Chadema, vijana hao walisikika
wakiimba wimbo unaosema ‘Bado wa wanamuamini Lowassa’ huku wakimtaka aungane
nao katika chama hicho walichoingia ili wakakamilishe sfari yao ya matumaini.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Mwenyekiti wa Jimbo Kinondoni, Waziri Muhuzi, anawakaribisha vijana hao
ili waweze kuungana na wezao kwa lengo la kukiondoa CCM madarakani na kuwaletea
maendeleo wananchi.
Alisema licha ya vijana hao kutoridhishwa na mchakato huo,
naye kada wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alikaririwa navyombo vya
habari kwamba alisekiktishwa na mnamna Kati ya Maadili ilivyoongozwa na
viongozi wasiofuata maadilikatika kufanya uteuzi na kusababisha kuvuruga
mchakato mazima wa uteuzi nadani ya chama hicho.
Alisema kutona kubaini ubabaishaji huo alimshauri Ngombale
Mwiru kujiunga kujiunga na Chadema ili waweze kusimamia maadili nchini.
“Aige mfano wa mkongwe mwenzake wa siasa za Zanzibar,
Hassan Moyo ambaye aliachana na CCM, hivi za sasa amekuwa akitoa ushauri kuhusu
masuala ya Zanzibar,”alisema Muhuzi.
Awali, kiongozi wa kikundi cha Wanavyo hao, Michael
Litanda, alisema kuwa wameamua kujiunga na Chadema kwa vile chama hicho ni basi
la kuwapeleka sehemu fulani, wakati kwa upande wa CCM safari yake imefika
kikomo.
“Tumezunguuka Tanzania nzima katika kuwashawishi wananchi
wakubali kumdhamini kada wetu kwa hiyo, sisi baada ya kuvurugika mchakato ule
tumehamia Chadema, kwa hiyo tunaomba aungane nasi,”alisema Litanda.
No comments:
Post a Comment