KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 10 August 2015

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAONGEZEKA

Mkurugenzi Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na makazi, Ephraim Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi julai umeongezeka kwa asilimia 0.4 kutoka asilimia 0.2 ya mwezi juni mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, ongezeko hilo limetokana na  kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula .
Alizitaja baadhi ya bidhaa hizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei pamoja na asilimia zake ndani ya mabano, kuwa ni unga wa mahindi (2.5), ulezi (2.5), samaki (4.8), viazi vitamu (2.6) na ndizi za kupika (3.4).
Kwesigabo alisema kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula ni gesi ya kupikia (3.7), dizeli (5.9) na petroli (4.9).
Aidha, mfumuko wa bei kwa nchi jirani umeongezeka kutoka asilimia 4.9 hadi 5.4, kwa Uganda ambapo nchini Kenya umepungua kutoka asilimia 7.03 hadi 6.62.

Hata hivyo, Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya Tanzania imefikia shilingi 62.na senti 98 julai mwaka huu ikilinganishwa na  septemba 2010.

No comments:

Post a Comment