WATU milioni 1.3 wanapoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na ajali za
barabarani, huku Tanzania ikipoteza watu kati ya 3500 hadi 4000 kwa mwaka.
Kati ya watu
hao, watoto zaidi ya laki tatu hupoteza maisha na wengine 20 wakibaki walemavu.
Hayo
yalibainishwa jijini Dar es Salaam leo, Ofisa mradi wa Usalama barabarani toka Shirika la Afya Duniani (WHO), Mery Kessiy,
wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wahabari juu ya Usalama Barabarani.
Mafunzo hayo
ambayo ni ya siku mbili yaliyoanza jana na kuhitimishwa leo, yameandaliwa
na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kufadhiliwa na WHO kwa kushirikiana na taasisi
ya Bringbeg.
Kessiy, alisema
ili kupunguza ajali za barabarani kuna haja ya jamii kuelimishwa hususani
kuvaa kofia, madereva waache kuendesha wakiwa wamelewa, kutumia vizuizi vya
watoto kwa uangalifu, kufunga mikanda na kupunguza mwendo kasi
Naye Mwanasheria
wa Kikosi cha Usalama barabarani (T), Trafiki Makao Makuu, Insp. Deus
Sokoni, alisema mkoa unaoongoza kwa ajali hapa nchini ni Kinondoni na sababu za
msingi kwa kuwa ndiko kwenye uchumi mkubwa kuliko mikoa mingine nchini.
“Starehe za
ajabu zinapatikana Kinondoni, hawajali
sheria za Usalama barabarani, hii inasababishwa na maendeleo ya
kiuchumi”alisema Insp. Sokoni.
Alitaja
mikoa yenye ajali chache kuwa ni Tanga, Njombe, Simiyu na Katavi na kudai kuwa
mkoa wa Tanga ajali ni chache kutokana
na kujitahidi kufuata sheria.
Alitaja
idadi ya ajali zilizotokea mwaka 2013 kuwa ni ajali 23,842 na zikasababisha
vifo vya watu 4002 na kuacha majeruhi 20,689 na mwaka 2014 ajali zilipungua na
kufikia 13,466 ambapo idadi ya vifo vilikuwa 3437 huku majeruhi wakiwa 13,465.
Insp. Sokoni,
alisema kikosi cha usalama barabarani
kimeweza kukusanya Sh 19,504,01 kwa mwaka 2013 na mwaka 2014 kimekusanya Sh. 29,926,77 kutokana na makosa ya
barabarani.
Alisema, kwa
sasa wamependekeza Serikali itunge sheria itakayowezesha kuwawajibisha madereva
wote wanaopenda kutumia simu wakati wanaendesha vyombo vya moto, wanaopakia abiria zaidi ya mmoja(mishikaki)
kwa wale madereva wa piki piki (bodaboda), kutovaa kofia na abiria wanaozidi
katika magari yaendayo mikoani.
“Hatutatoa
adhabu kwa madereva tu bali hata kwa
abiria atakayekutwa anavunja sheria” alithibitisha.
Aidha alitoa
wito kwa wananchi kutambua suala zima la
usalama barabarani kwa kuwa ni jukumu la kila mmoja na kudai
kuwa kila mmoja akitimiza nafasi yake hakika Tanzania itakua salama bila ajali.
Katika hali
ya kushangaza, Insp. Sokoni, alisema hakuna sheria inayozuia waendesha pikipiki
(Bodaboda), kuingia katikati ya jiji bali polisi wamekuwa wakiwakamata kutokana
na kushindwa kuvaa kofia ngumu (helmet).
Bodaboda
wamekuwa wakikamatwa kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadik,
lakuwataka wasiingie katikati ya jiji kwa madai kwamba wamekuwa wakishiriki
katika vitendo vya kihalifu.
Asante Sokoni,kwa kupendekeza sheria nzuri ila bado kuna jambo linatakiwa...
ReplyDeleteAsante Sokoni,kwa kupendekeza sheria nzuri ila bado kuna jambo linatakiwa...
ReplyDelete