KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 10 August 2015

WATU MILIONI 1.2 HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA

WATU  milioni  1.3 wanapoteza maisha  kila mwaka duniani kutokana na ajali za barabarani, huku Tanzania ikipoteza watu kati ya 3500 hadi 4000 kwa mwaka.
Kati ya watu hao,  watoto  zaidi ya laki tatu hupoteza maisha  na  wengine 20 wakibaki walemavu.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam leo, Ofisa mradi wa Usalama barabarani  toka Shirika la Afya Duniani (WHO), Mery Kessiy, wakati  akitoa  mafunzo kwa waandishi wahabari  juu ya Usalama Barabarani.
Mafunzo hayo ambayo ni ya siku mbili  yaliyoanza  jana  na kuhitimishwa  leo,  yameandaliwa na Wizara ya Afya na  Ustawi wa Jamii  na kufadhiliwa na WHO kwa kushirikiana na taasisi ya Bringbeg.
Kessiy,  alisema  ili kupunguza ajali za barabarani kuna haja ya jamii kuelimishwa hususani kuvaa kofia, madereva waache kuendesha wakiwa wamelewa, kutumia vizuizi vya watoto kwa uangalifu, kufunga mikanda na kupunguza mwendo kasi
Naye  Mwanasheria  wa Kikosi cha Usalama barabarani (T), Trafiki Makao Makuu, Insp. Deus Sokoni, alisema mkoa unaoongoza kwa ajali hapa nchini ni Kinondoni na sababu za msingi kwa kuwa ndiko kwenye uchumi mkubwa kuliko mikoa mingine nchini.
“Starehe za ajabu zinapatikana Kinondoni,  hawajali sheria za Usalama barabarani, hii inasababishwa na maendeleo ya kiuchumi”alisema  Insp. Sokoni.
Alitaja mikoa yenye ajali chache kuwa ni Tanga, Njombe, Simiyu na Katavi na kudai kuwa mkoa wa  Tanga ajali ni chache kutokana na kujitahidi kufuata sheria.
Alitaja idadi ya ajali zilizotokea mwaka 2013 kuwa ni ajali 23,842 na zikasababisha vifo vya watu 4002 na kuacha majeruhi 20,689 na mwaka 2014 ajali zilipungua na kufikia 13,466 ambapo idadi ya vifo vilikuwa 3437 huku majeruhi wakiwa 13,465.
Insp. Sokoni, alisema kikosi cha usalama barabarani  kimeweza kukusanya Sh 19,504,01 kwa mwaka 2013 na mwaka  2014 kimekusanya  Sh. 29,926,77 kutokana na makosa ya barabarani.
Alisema, kwa sasa wamependekeza Serikali itunge sheria itakayowezesha kuwawajibisha madereva wote wanaopenda kutumia simu wakati wanaendesha vyombo vya moto,  wanaopakia abiria zaidi ya mmoja(mishikaki) kwa wale madereva wa piki piki (bodaboda), kutovaa kofia na abiria wanaozidi katika magari yaendayo mikoani.
“Hatutatoa adhabu kwa madereva tu bali  hata kwa abiria atakayekutwa anavunja sheria” alithibitisha.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kutambua suala zima  la usalama  barabarani  kwa kuwa ni jukumu la kila mmoja na kudai kuwa kila mmoja akitimiza nafasi yake hakika Tanzania itakua salama bila ajali.
Katika hali ya kushangaza, Insp. Sokoni, alisema hakuna sheria inayozuia waendesha pikipiki (Bodaboda), kuingia katikati ya jiji bali polisi wamekuwa wakiwakamata kutokana na kushindwa kuvaa kofia ngumu (helmet).

Bodaboda wamekuwa wakikamatwa kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadik, lakuwataka wasiingie katikati ya jiji kwa madai kwamba wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya kihalifu.

2 comments:

  1. Asante Sokoni,kwa kupendekeza sheria nzuri ila bado kuna jambo linatakiwa...

    ReplyDelete
  2. Asante Sokoni,kwa kupendekeza sheria nzuri ila bado kuna jambo linatakiwa...

    ReplyDelete