KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 20 January 2016

KIBAMBA KIMBILIYO LA VIBAKA

WAKAZI wa Kibamba wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameliomba Jeshi la Polisi kuwakamata vibaka waliyoibuka kama uyoga katika eneo hilo, kuwafikisha katika vyombo vya sheri.
Wakazi hao, waliyasema hayo wakati walipozungumza na mwandishi wa SAUTI PEVU jijini jana, kwamba hivi sasa wanaishi kwa wasiwasi  kila linapoingia giza.
Walisema eneo hilo la Kibamba hivi sasa limekumbwa na vitendo vya uhalifu kutokana na vijana wengi waliyokimbilia huko kujificha baada ya kufanya uhalifu katika maeneo mengine jijini.
“Hawa vijana wanaotusumbua wengi wao ni wale waliyofanya uhalifu katika maeneo mengine ambako wanatafutwa ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria lakini cha kushangaza baadala watulie lakini ndiyo kwanza wanaendelea na uhalifu wao tunawajua mmoja mmoja,”alisema mmoja wa wakazi hao huku akiungwa mkono na wenzake.
Walisema, baadhi ya vijana hao wapo wanatoka manzese, wakiiungana na wengine kutokea Maili Moja mkoani Pwani.
Pia walisema vibaka hao wamekuwa wakijeruhi wakazi wa maeneo hayo wakati wanapovamia nyumba, kwa lengo kupatiwa kile wanachohitaji.


 

No comments:

Post a Comment