KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 20 January 2016

WAZAZI WAHOJI MICHANGO WANAYOTOZWA



WAZAZI na walezi wa wanafunzi wa Shule ya Wasichana Nyabkubu, mjini Geita wamelalamikia michango wanayotozwa kwa ajili ya chakula.
Wakizungumza nje ya ukumbi wa shule hiyo muda mfupi baada ya kikao chao na Ofisa Elimu Mkoa pamoja na mwalimu mkuu wa shule hiyo walisema wanashangazwa kuambiwa watoe 450,000. 
“Tumetangaziwa elimu ni bure nchi nzima kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari lakini tunashangazwa tumeitwa na kuambiwa tunatakiwa kutoa 450,000 kwa ajili ya chakula tuna mashaka huenda wanataka kutuchakachua,”alisema Janes.
Akijibu malalamiko hayo, Ofisa Elimu Mkoa wa Geita, Rehema Mbwilo, alisema wazazi wanatakiwa kutimiza wajibu wao kwa kuwahudumia chakula watoto wao wanaosoma bweni kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
Mbilo aliongeza kuwa shule ya wasichana Nyankumbu imesajiliwa kama shule ya kutwa kwa kidato cha kwanaza na cha nne isipokuwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ndio serikali inagharimia chakula na ada.

No comments:

Post a Comment