MWALIMU wa shule ya msingi Ikombolinga Peter Emma, ameeleza masikitiko
yake ya kudhalilishwa na Ofisa Elimu wa shule ya msingi, Mohammed
Msongo, wilaya Chamwino kwa kuzabwa makofi na mwalimu huyo mbele za walimu
wenzake. Mwalimu Emma alisema udhalilishaji aliofanyiwa na Ofisa
elimu huyo kwa kupigwa makofi mbele za walimu wenzake unatokana na
kuchelewa kufika katika semina ya mafunzo ya KKK licha ya kuwa mwalimu
huyo alikuwa anatoka mbali na alikuwa hajalipwa fedha za nauli. Akielezea
tukio hilo mwalimu Emma alisema kwa mujibu wa ratiba ya mafunzo
ambayo yalianza 16 Januari mwaka kuu yalitakiwa kuanza saa mbili kamili
lakini yeye na wenzake zaidi ya 20 walifika saa 2:40 asubuhi. Akiendelea
kuzungumza na waandishi wa habari mwalimu huyo alisema, kwamba yeye na
walimu wenzake waliochelewa na walimkuta Ofisa Elimu Msingi, Mohammed
Msongo, ambaye aliwazui kuingia darasani kutokana na kuchelewa kwao. Alisema
Ofisa huyo aliendelea kuwakaripia na kuwataka waandike majina yao kwa
malengo kwamba wasihudhurie mafunzo hayo KKK ambayo yalikuwa yanawahusu
walimu wote wa darasa la kwanza na la pili. "Wakati najitetea kuwa
tunatoka mbali na usafiri ni wa shida huku hatukuwa na hela Ofisa Elimu
alinizaba makofi na kunisukuma ukutani. "Kitendo hicho kweli kimeniumiza na kunidhalilisha sana hata hapa najifunza lakini sina amani natamani kurudi nyumbani. "Tuliandika
majina ya waliochelewa sijui tutalipwa au la maana tunatakiwa kulipwa
sh. 55000 kwa kila siku nne pamoja na nauli lakini mpaka sasa hatujalipwa
mimi sielewi kwakweli nimefadhaika sana.
"Kama uongozi ni wa ubabe hivyo hakika kazi itakuwa ngumu sana kwani hali hii inavunja moyo"alisema Mwalimu Emma. Kwa
upande wake Kaimu mkurugenzi wa Chamwino Richard Masimba alipotafutwa
ofisini kwake alisema taarifa hizo hawana na watazifuatilia. Masimba
alisema ofisi haina taarifa ya mwalimu kupigwa vibao na kusukumwa
ukutani na iwapo itathibitika hatua za kisheria na kinidhamu zitafanywa.
Akizungumzia
suala hilo, Ofisa Elimu Msingi wilaya ya Chamwino, Mohammed
Msongo, alikana na kukataa kata kata kwamba yeye hajampiga kibao wala
kumsukuma ukutani mwalimu huyo. "Jumla ya walimu 348 wanapatiwa mafunzo kazini na mafunzo hayo ni kwa shule za msingi serikali 119.
"Ila
ni kweli wapo walimu waliochelewa badala ya kufika saa 2:00 kama
tulivyo kubaliana wao wamefika saa 2:40 hivyo walipoteza dakika 40 za
kipindi."Kutokana na hali hiyo nililazimika kukaa na walimu wote
waliochelewa yakiwa makundi mawili na kuwapa maelekezo ili wasiendelee
kuchelewa kwani kwa kufanya hivyo hawawezi kufaidika na hayo
masomo"alijieleza Msongo.
Hata hivyo Msongo alisema siku ya
tukio ambalo inadaiwa alimpiga mwalimu huyo alimshika shati kwa nyuma na
kumvuta ikiwa ni hatua ya kutaka asijichanganye na kundi lingine lisilo
muhusu lakini siyo kumpiga.Kwa upande wake Katibu wa Chama cha
Walimu (CWT), wilaya ya ChamwinoJames Puya alisema analaani vikali
kitendo cha Ofisa Elimu msingi kumzaba mwalimu vibao."Kitendo hicho kinawafanya watumishi kukosa morali wa kufanya kazi kwa ufasaha na wakati mwingine kuhamishia hasira kwa watoto."Mimi
nimepata taarifa za mwalimu kupigwa na nasema kama kiongozi wa CWT
wilaya ya Chamwino kulikotokea hili tatizo naomba tume ya Haki za Binadamu, Mkurugenzi na Utumishi kuingilia kati suala hili."Unyanyasaji
huu usipokomeshwa haraka itakuwa mwendelezo wa viongozi wa ngazi ya juu
kuwanyanyasa watumishi wa ngazi ya chini jambo ambalo ni hatari"alisema
Puya.
No comments:
Post a Comment