KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday, 23 February 2016

MUHABHI:HATUTASHIRIKI UCHAGUZU WA MARUDIO ZANZIBAR



CHAMA Cha Kijamii (CCK), kimeshangazwa na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kwa kukitaja chama hicho kwenye orodha ya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi wa marudio Machi 20, mwaka huu.
Kauli hiyo ya CCK imekuja baada ya ZEC juzi kuvitaja vyama vitakavyoshiriki katika uchaguzi huo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muhabhi, aliitaka ZEC kuheshimu uamuzi wa chama chake ambacho kinaongozwa na katiba moja.
Muhabhi, alishangazwa na uamuzi huo kwa kuwa chama hicho tayari kimekwisha kutangaza msimamo wake ambao ni kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.
Alisema hawakubaliani na tamko hilo la Jecha, kwa kuwa vikwazo vilivyokwamisha uchaguzi wa awali bado vipo, hivyo hakuna haja kwa chama chao kushiriki uchaguzi huo ambao matokeo yake yanafahamika.
“Tamko hilo la Jecha amelitamka yeye, sisi tutakutana na tutalitolea tamko, kama unavyojua kuhusu uchaguzi huo tumekubaliana na baadhi ya makatibu wakuu wa vyama kukutana kisha tutatoa tamko la pamoja,” alisema.
Muhabhi alisema Jecha hana haki ya kulazimisha fikra zao na kuwazungumzia watu, kwa kuwa vyama ni taasisi, vina kanuni na taratibu zake za kujiendesha.
“Anatangaza kuwa tunashiriki wakati anajua fika kwamba kuna hoja zetu tulizowaandikia ambazo hadi sasa hajazijibu, kwa hiyo tutakutana haraka kutoa tamko letu kuhusu tamko lake,” alisema.
Aliwataka ZEC kutambua kuwa CCK ni chama kimoja, uamuzi ukipitishwa ni wa nchi nzima na hakuna wa kuugeuza.

No comments:

Post a Comment