KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 26 February 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA MSAADA WA VIFAATIBA VYA KISASA KUTOKA KAKPUNI ZINAZOTENGENEZA VINYWAJI BARIDI

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa ameitaka Bohari ya Dawa nchini (MSD), kuwa inahakikisha inavifikisha salama msaada vifaatibaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 10, ambavyo vimetolewa na Kampuni zinazozalisha vinywaji baridi kwa ajili ya hospitali za mikoa 14.
Hata hivyo hafla hiyo iliingia dosari baada waziri mkuu kuzuiliwa na wafanyakazi wa PSI asiondoke hadi asikilize kilio chao cha manyanyaso wanayofanyiwa na uongozi wao.
Majaliwa aliyasema hayo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaatiba hivyo, kwamba vimekuja katika wakati muafaka kwani msaada huo utasaidia katika kukabiliana na upungufu wa vifaa na vifaatiba vya kutolea huduma za afaya.
Msaada huo umetolewa na Kampuni zinazotengeneza vinywaji baridi ambazo ni Coca Cola Kwaza (T), Nyanza Bottlers; Bonite; Kampuni ya SBC-Pepsi (T); Kampuni ya SSB (Azam) na nyingine.
Alisema lengo la msaada huo ni kwenda kwenye vituo vilivyokusudiwa kwa hiyo serikali haitakubali kuona baadhi ya watu wasiyokuwa waaminifu wanavuruga mpango uo kwa kuviharibu au kuiviiba kwa masilahi binafsi
“Niambiwa vifaa na vifaatiba vitakavyokabidhiwa vina thamani ya shilingi bilioni 10 za kitanzania ambayo ni makontena 20 yenye refu wa futi 40 kila moja ambayo ndani yake kuna makasha zaidi ya 1,500 ya vifaa vipya kabisa na vingine zaidi ya 300 vikiwemo vitanda 80 na magodoro yake.
“Msaada huu ni mkubwa ambao haujawahi kutokea katika sekta ya Afya, napenda kutumia fursa hii kusistiza kwamba serikali kupitia MSD, itahakikisha vifaa hivi vinasambazwa kwenda kwenye vituo husika kwa umakini mkubwa ili viweze kutumika kama ilivyokusudiwa”alisema Majaliwa.
Aliyataja orodha ya maeneo ambayo yana upungufu wa vifaa na vifaatiba, ambako wanatarajia kuvipeleka kuwa ni Mikoa ya Dodoma, Geita, Katavi, Kilimanjaro, Kigomana naLindi.
Mingine ni Mara, Mbeya, Mtwara, Shinyanga, Tanga, Tabora na Rukwa huku akibainisha kuwa kutokana na mzigo huo kuwa mkubwa anaamini kuwa mikoa yete iliyobaki ya Pwani, Singida, Iringa yote inaweza kupata.
Aidha, Majaliwa alisema kindo hicho ni ishara kuwa mabadiliko nmakubwa yanaweza kutokea nchini, ikiwa serikali na sekta binafsi watafanya kazi pamoja kam ilivyojitokeza.
Majaliwa, aliongeza kwa kusema kuwa serikali itaendelea kuboresha uhusiano na ushirikiano na sekta binafsi katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Wafanyakazi wampokea kwa mabango
Wakati akiwa anaondoka kundi kubwa la wafanyakazi wakiongozwa na mtu mwenye ulemavu, walifunga barabara kuzui waziri ili aseme chochote kuhusu haki zao ambazo zinafinyangwa.
Waziri Mkuu baada ya kuzuiwa ilibidi shuke kwenye gari ili kuwasikiliza, ndipo kiongozi wa wafanyakazi hao, Amin Athuman alipoanza kueleza uneovu wanaofanyiwa.
Alisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu bila ya kupewa mikataba huku wanacholipwa hakiendani na kazi wanazofanya.
“Hapa sisi kila tunapodai haki zetu tunatishiwa kufukuzwa kazi, hatuna PPF kwa Ujumla uongozi ni mbovu kwani hata usalama wetu kaazini uko mashakani tuna kuomba utusaidie kwa vile serikali yako imeonesha kusaidia wanyinge na tuna imani nayo,”alisema Athuman.
Baada ya kumaliza kuelezea kero zao, Majaliwa, aliwataka wafanyakazi hao wafifike kazini leo ya kukosa kwani atamwaaiza waziri mwenye dhamana Jenista Mhagama afike ofisini hapo kwa ajili ya kuwasikiliza.
“Mmsema hamna makato ya PPF, niwaahidi hidi kuwa kesho (leo), atakuja kulishughulikia tatizo lenu na kwa kawaida hatucheleweshi kumaliza matatizo, kwamba matatizo  yenu yote yatapatiwa ufumbuzi hapo hapo,”alisema Majaliwa.
Alipomaliza kusema hayo aliwaomba wampishe ili apate kuondoka, bila kipingamizi alipishwa na kuendelea na safari.
Awali, Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, alisema anazishukuru kampuni hizo kwani zimekuwa mfano wa kuigwa huku akibainisha kuwa MSD imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na kampuni ya Coca Cola kwa muda mrefu sasa.
Alisema licha ya kampuni hizo kutoa msaada huo bado pia zimeahidi kutoa msaada wa mafunzo kwa watanzania watakaosimamia vifaa hivyo kwa gharama zao.
Pia, aliiomba serikali kiongezea bajeti ili iweze kusimamia mipango yake ya kuboresha huduma za afya nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadizios, aliipongeza serikali katika hatua zake za kupambana na vitendo vya rushwa nchini.
Alisema hali hiyo itaweza kuifanya Tanzania ifanikiwe katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment