KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Saturday, 27 February 2016

SERIKALI IIREJESHE HOTEL YA EMBASI KATIKA HIMAYA YAKE



SERIKALI imetakiwa kuchunguza mkataba wa muwekezaji katika Hotel ya Embasy ili kubaini kama ameshindwa kuiendeleza basi irudishwe serikalini kwa ajili ya masilahi ya Taifa.
Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana, Rais John Magufuli, aliahidi kurudisha viwanda ma maeneo mengine ambayo wawekezaji wake wameshindwa kuyaendeleza huku wemgine wakigeuza kazi za mikataba waliyokubaliana na serikali.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivukoni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, Gesper Makame aliyasema hayo jana, wakati alipokuwa akizungumzia taarifa za kuwa muwekezaji katika hotel hiyo, ameanzisha gereji bubu ambayo inadaiwa kuwa kero kwa baadhi ya ofisi za jirani.
Alisema hayo baada ya wakazi wengi wa mtaa huo kuhoji kuwa inakuwaje mradi wa kuendeleza hoteli hiyo unaendeshwa kwa kusuasua na umechukua muda mrefu, huku wakidai kuwa eneo hilo hivi sasa limegeuzwa kuwa gereji bubu kinyume cha sheria.
Hata hivyo, Makame, alisema hatua hiyo ya kuiresha serikalini itafuatia baada ya serikali kuchunguza na kujiridhisha kama muwekezaji huyo ameshindwa kutekeleza  vigezo vya mkataba aliyoingia ns serikali.
“Nikweli nilipokea malalamiko hayo kuwa pale kumeanzishwa gereji bubu hali iliyonifanya niende na kukutana nawasimamizi wa hoteli hii ambao tulikubaliana kuwa wasingeendelea na utaratibu huo, nikweli kuna gari nimeiona ambayo bodi yake ilikuwa ikitengezwa.
“Kwanza ni kinyume cha sheria isitoshe jirani zao wanalalamika kuwa wanawasumbua kwa kelekele wakau wamatengenezo hayo ya magari hivyo kuwafanya wakose utulivu wa kutekeleza majukumu yao,”alisema Makame.
Alisema kutokana na mazungumzo hayo, aliamini kuwa hawangeendelea tena, sasa kama wanaendelea kama inavyodaiwa na majirani zao basi atayafanyia kazi madai hayo.
Naye Ofisa Utawala wa Kampuni ya Wellworth Group, ambao ndiyo wamiliki wa Hoteli hiyo, Simon Nguka, alisema madai hayo hayana ukweli wowote, kwamba madai hayo yanalengo la kutaka kuupotosha umma kuhusu mradi mkubwa ambao utakuwa chanzo kizuri cha mapato kwa taifa.
“Magari yaliyoko pale ni ya kampuni kwa hiyo siyo kweli kama kuna gereji bubu, hizi taarifa hazina ukweli waowote na waliyozitoa hawajui chochote kuhusu kinachoendelea pale,”alisema Nguka.
Pia, alipinga na kuwashangaa wanaodai kuwa huenda kuchelewa kukamilika kazi ya ujenzi huo kumetokana na wamiliki wake kuzitumia hati za umiliki wa jengo hilo kwenda kukopa fedha kisha kuzitumia katika miradi yao mingine, na kuwataka wenye ushahidi wa hilo waupeleke serikalini.
Alisema hakuna kitu kama hicho kinachoendelea ni majungu kutoka kwa watu ambao hawana ufahamu  na uwekezaji huo, ambapo naamini serikali ndiyo inajua ukweli wa uwekezaji huo.
MWISHO

No comments:

Post a Comment