KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 24 March 2016

DK. DELILA AHUZUNIKA MBELE YA KAMATI YA UKIMWI



KAMATI ya Bunge ya Ukimwi imeibu madudu katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kubaini kitanda kimoja hutumika kulaza watoto 15 kwa wakati mmoja.
Kaimu Mganga Mkuu Delila Mushi alieza hayo mbele ya Kamati hiyo wakati ilipofanya ziara ya kushtukiza kataika Hospitali hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza kwa hisia mbele ya Kamati hiyo Dk Delila alisema katika wodi ya watoto kuna vitanda 18 ambapo watoto  wachanga 150 hulazwa katika vitanda 10 sawa na watoto 15 kitika kila kitanda kimoja.
“Wakati watoto hao wakilala kitandani wazazi wao wanalala chini jambo ambalo linatusikitisha,”alisema Delila.
Alisema hali hiyo imechangiwa wodi ya watoto kukosa nafasi ya kuongeza vitanda kwa vile hakuna nafasi kwa muda mrefu sasa.
DK. alisema katika vitanda hivyo 18, kuna vitanda nane vimetengwa kwa ajili ya watoto njiti.
“Hili suala tayari tumekwisha liandikia barua kwa muda mrefu lakini hadi sasa bado tunasubiri utekelezaji kutoka serikalini,”alisema Dk. Delila.
Dk. Delila, alisema nafasi ya kujenga jengo jipya ipo na baadala yake imekuwa ikitumia majengo ya zamani ambayo hayo hayaendani na ongezeko la wakazi.
“Hivi sasa hospitali hii inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ya majitaka hali inayosabisha kufurika na kusambaa harufu katika hospitali hiyo,”alisema Dk. Delila.
Aidha, Dk. Delila, alisema pia wanakabiliwa na tatizo la mashine ya kuchakata takataka kwani iliyopo uwezo wake ni wa kuchakata kilo 120 huku hospitali hiyo ikizalisha kilo 200 kwa siku.
Alisema gharama ya kununua mashine hiyo ni sh. milioni 100.   
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa wafanyakazi ambao ni tatizo kubwa linalo ikabili hospitali hiyo kwa muda mrefu sasa.
Akizungumzia Changamoto hizo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Husna Mwilima, alisema ingawa ziara yao ilikuwa ikilenga zaidi kutembelea kitengo cha dawa za kulevya, hata hivyo suala la afya ni la kila mdau kwa hiyo wanamuahidi kuwa watalifuatilia suala hilo.
“Kwa kweli jambo hili limetusikitisha, kwa ulivyolizungumzia inaonesha ni jinsi gani unavyoumia na kutufanya hata sisi tujisikie huzuni kwa hiyo Kamati yetu itahakikisha ufumbuzi wa matatizo yote hayo yanapatiwa ufumbuzi wa haraka,”alisema Husna.
Kwa upande wake Dk. Hassan Nyandindi, alisema tangu kuanzishwa kitengo cha Methadine mwaka 2012, hivi sasakitengo hicho kinahudumia waathirika 1110 kati ya hao wanawake ni 179.
Kwaa upande wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika Kitengo cha Mihadarati, Dk. Jessie Mbwambo, alisema wasichana wako wanaotumia mihadarati wako hatarini kuambukizwa na kuambukiza ugojwa wa ukimwi kwa vile wamekuwa wakifanya mapenzi na wanaume 60 kwa mwezi.
Alisema kutokana na matumizi hayo ya dawa za kulevya wanawake hao wamejikuta wakiingia katika vitendo hivyo bila ridhaa yao.
Alisema kutokana na mazingira hayo, inafanya wasichana hao kuwa chanzo cha maambukizi mapya ya Ukimwi.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dk. Abdallah Possi, alisema ili kupambana na matumizi ya mihadarati kuna haja ya Wabunge kuisaidia serikali kuwafichuwa vigogo wanaohusika na biashara hiyo.
"Ni waombe bajeti ya wizara yetu itakapowasilishwa bungeni muingune mkono ili kuondoa matatizo katika sekta ya afya,"akisema Dk.Possy.
Vilevile aliwatahadhalisha wabunge kuwa wanaweza kujikuta wanashindwa kuwataja baadhi ya wafanyabiashara wanaowasaidia labda nyakati za kampeni hivyo kujikuta wakipatwa na kigugumizi cha kuwataja kwani baadhi yao ndiyo hao hao wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.
Pia alisema matatizo yote yaliyoainishwa na Vitengo hivyo vya dawa za kulevya yani kile cha Muhimbili na Mwananyamala, ameyachukua na kwenda kuyafanyia kazi kwa kushirikiana Wizara ya Afya.
Pia aliwakumbusha wabunge hao kuwa mipango ya serikali ya awamu ya tano ni kuondokana na bajeti tegemezi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment