KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 28 March 2016

TANZANIA YAPATA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA LA KUTOKA UGANDA HADI BANDARI YA TANGA



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, amesema Tanzania inayo nafasi kubwa ya kupata mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga ukilinganisha na nchi nyingine zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Profesa Ntalikwa, alisema hayo, baada ya makubaliano kati ya Tanzania na Uganda, ya kujenga bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,410; Kenya ikaibuka na kuanza kufanya mikakati kwa kasi ya ajabu wakitaka mradi huo upitie bandari ya Lamu.
Kama hiyo haitoshi, Katibu Mkuu wa wa Nishati wa Kenya alikamatwa na maofisa Uhamiaji mkoani Tanga baada ya kujaribu kujipenyeza kwenye ujumbe wa Waziri wa Nishati wa Uganda, uliyokuja nchini kuangalia mazingira ya utekelezaji mradi huo bandani Tanga.
Akizungumza na wandishi wa habari nje ya mkutano kati ya Wizara hiyo na wafanya biashara wa Sekta ya mafuta nchini, ambao ulifanyika jijini Dar es Salaam jana, Profesa Ntalikwa, alisema lengo la kukutana na wafanyabiashara hao ni kuwatangazia fursa zinazoweza kupatikana katika mradi huo mkubwa.
Alisema kujengwa mradi huo, kunatokana na mazingira ya Tanzania ikiwemo usalama katika ardhi yake, yanatoa fursa kubwa kufanikisha mradi huo ukilinganisha na nchi nyingine.
“Tanzania ina uzoefu wa kuendesha miradi mikubwa kama hiyo, mfano ni miradi ya mabomba manne gesi ambayo tunayo kwa sasa,”alisema Profesa Ntalikwa.
Pia Profesa Ntalikwa, alisema vigezo vyote vinavyohitajika katika ujenzi huo ikiwemo bandari yenye kina kirefu ipo katika mkoa huowa Tanga linako tarajiwa kujengwa.
“Ujenzi wa mradi huu utagharimu sh. Bilioni nne hadi kukamilikakwake kwani unatarajiwa kuanza mwaka ujao kisha kukamilika ndani ya miezi 36,”alisema Profes Ntalikwa.
Akizungumzia kushirikishwa wafanyabiashara hao Profesa Ntalikwa, alisema lengo la kukutana nao ni kuwatambulisha fursa nyingi za kibiashara, ambazo zitapatikana katika mradi huo.
“Mradi huu ni mkubwa na una manufaa makubwa kiuchumi kwa taifa hivyo, ni lazima kila mfanyabiashara na raia kwenye nafasi yake ungane na serikali kuhakikisha hautoki mikononi mwetu kwani tayari mkuu wan chi ameonesha dhamira ya dhati kuhakikisha Tanzania inasonga mbele,”alisema Profesa Ntalikwa.
Alitaja faida hizo za kiuchumi kuwa ni upatikanaji wa zabuni kubwa, utazalisha ajira, kodi mbalimbali ambazo zinaweza kupatikana lakini bomba hilo litakuwa na faida na faida kuchechemua pato la nchi.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao, Gideon Kaunda, alisema baada ya mkutano huo watasafiri kwenda nchini Uganda kukutana na Rais Yoweli Museven kumuelezea kuwa Tanzania ndiko sehemu ambayo inaweza kujengwa bomba hilo.
Alisema kuwa wafanyabiashara wote wa sekta ya mafuta nchini  wamejidhatiti kwa ajili ya kupokea mradi huo na hawako tayari kuponyokwa, kikubwa wanaomba ushirkiano kati yao na serikali ili kukamilisha adhima ya mradi huo.

No comments:

Post a Comment