Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
akifungua jengo la Maabara la Shule ya Sekondari ya Mwakaluba katika
jimbo la Kisesa akiwa aktika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu , Dkt Titus Kamani na
Wazpili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano
na Mazingira, J. Mpina. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua maabara ya Shule ya Sekondari ya Mwakalubi katika jimbo la
Kisesa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016 (picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
akikagua shamba la pamba la mfano la mkulima Gamuga Kimali kqtika
kijiji cha Nandoya wilayani Meatu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipongeza Mama Anastazia Petro kwa kujifungua salam motto wa kiume
aliyepewa jina la Majaliwa wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha
Mwandoya akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
akiteta na Waganga na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Mwandoya wilayani
Meatu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Nandoya
wilayani Meatu baada ya kuzindua jengo la upasuaji na kusalimia wagonjwa
akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa Simiyu ili wakae na
uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili kubaini tatizo la mipaka
baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa
vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku ya tano ya ziara yake
mkoani Simiyu.
“Tangu niingie hapa mkoani
malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali nilikopita. Nimeamua
kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili ua Utalii, Profesa
Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. George
Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo yenu,” alisema.
“…Nitawatuma waje na wapite kila
wilaya, wakae na kuzungumza na wakulima na wafugaji ili kubaini ni
chanzo cha tatizo la migogoro hii kwenye mipaka ya vijiji na hifadhi ya
Serengeti. Pia Waziri wa TAMISEMI itabidi atoe ufafanuzi kuhusu agizo
lao la kutofanya shughuli yoyote mita 60 kutoka kwenye mto Simiyu ili
wananchi waelewe,” alisema.
Mapema, Mbunge wa Kisesa ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira) alimweleza waziri Mkuu
mbele ya wananchi hao kwamba limetolewa zuio linalowakata wakazi wa mkoa
huo wasifanye shughuli zozote umbali wa mita 60 kutoka kwenye kingo za
mto huo.
“Limebandikwa tangazo
linalokataza wananchi waishio kando ya mto Simiyu wasifanye chochote
kuanzia Julai 30, 2016. Wananchi hawajashirikishwa wala kuelezwa
chochote zaidi ya kuona bango la matangazo tu. Watu wananakatazwa
wasichote maji wala kunywesha mifugo wakati hakuna mabwawa,
itawezekanaje? Tunaomba kauli yako kuhusu jambo hili,” alisema.
Ili kumaliza tatizo la migogoro
ya ardhi hapa nchini, Waziri Mkuu alisema Serikali ina mpango wa kuunda
mabaraza ya ardhi 100 kwa nchi nzima ambayo yatakuwa na jukumu la
kutatua migogoro ya ardhi kwa wakati
Akitoa taarifa ya wilaya hiyo,
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Bw. Erasto Sima alisema wilaya hiyo
iliyoanzishwa Julai mosi, 1987 ina ukubwa wa kilometa za mraba 8,835
ambapo asilimia 49 (sawa na kilometa za mraba 4,329) ya eneo lote la
wilaya hiyo ni hifadhi za wanyamapori.
Alilitaja eneo hilo kuwa ni pori
la akiba la Maswa, sehemu ya hifadhi ya Serengeti, Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro na pori la hifadhi ya usimamizi wa wanyama (WMA) la Makao na
kwamba asilimia 51 iliyobakia indiyo inayotumiwa kwa makazi ya watu,
kilimo na malisho ya mifugo.
No comments:
Post a Comment